Jumamosi, 16 Agosti 2014

Wahamiaji haramu 21 wanaswa wakiwa ndani ya roli la saruji


 
 Naibu Kamishna uhamiaji mkoa wa Njombe Bi. Rose Mhagama akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake.


  Baadhi ya wakazi wa mjini Makambako Mkoani Njombe waliojitikeza kuwaangalia wahamiaji hao( kulia) na waliokaa ni raia wa Ethiopia mara baada ya kukamatwa na kufikishwa katika ofisi za uhamiaji za Makambako. 

Na James Festo, Njombe.

IDARA ya Uhamiaji Mkoani Njombe, imefanikiwa kuwanasa wahamiaji haramu 21 walioingia nchini kwa kutumia roli la kubebea mifuko ya saruji ambalo lilikamatwa na maofisa uhamiaji katika eneo Mashujaa kwenye Halmashauri ya Mji wa Makambako.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Naibu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Mkoani Njombe, Rose Mhagama alithibitisha kukamatwa na kushikiliwa kwenye kituo cha polisi Makambako wahamiaji hao ambao ni raia wa kutoka nchini Ethiopia.

Mhagama alisema askari wa kikosi cha uhamiaji mnamo Agosti 14,mwaka huu majira ya saa 12:30 jioni wakiwa kwenye doria katika barabara kuu ya kutoka Makambako kwenda Songea walilishuku na kulisimamisha roli namba T587 CSN likiwa na tela namba T780 CHM lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Nyange na kuanza kulikagua.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni