Wajakazi Brazil wapata
afueni
Sheria mpya ambapo waajiri watatozwa faini
iwapo watashindwa kuwasajili kwa mikataba wafanyikazi wao wa nyumbani imeanza
kutekelezwa nchini Brazil.
Ni miongoni mwa hatua mpya zinazolenga kuwalinda wafanyakazi hao
wapatao milioni sita.
Mwaka uliopita marekebisho ya kikatiba yaliwapa wafanyakazi wa
nyumbani takriban saa 44 za kufanya kazi kwa wiki. Waajiri sasa wanaweza
kupigwa faini ya mamia ya dola kila mara wanapokiuka sheria hiyo.
Sheria hiyo mpya imesababisha familia nyingi kuwaajiri
wafanyikazi zaidi ili kufanya kazi kwa zamu huku waajiri wakilazimika kufanya
kazi za ziada.
Mwaka jana mageuzi ya kikatiba yaliwawezesha wafanyakazi wa
nyumbani kufanya kazi kwa masaa 44 kwa wiki.
Pia walipata haki nyinginezo kama kufanya kazi kwa saa nane kwa
siku , kupata kiwango kizuri cha mshahara, kupumzika wakati wa mchana, kulipiwa
malipo ya uzeeni na faida nyingiezo.
Sehemu kubwa ya mabadiliko haya imetekelezwa lakini bado kuna
changamoto.
Ikiwa mfanyakazi atafutwa kazi bila sababu , basi mwajiri wake
atalazimika kulipa asilimia 40 zaidi ya mshahara wake pamoja na asilimia
nyingine kumi kwa serikali.
Sheria hizi bila shaka zimefanya hali kuwa ngumu kwa wajiri na
hivyo baadhi yao wanajifanyika kazi zao.
BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni