Drogba alisaidia nchi yake katika upatanishi baada ya
mgogoro wa kisiasa
Mchezaji soka maarufu wa Ivory Coast Didier Drogba,
ametangaza kustaafu kutoka katika soka ya kimataifa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, alichezea Ivory Coast
zaidi ya mara miamoja.
Alishiriki kombe la dunia mara tatu na mashindano ya kombe la
Afrika mara 2
Amesema kuwa anajivunia kusaidia nchi yake kufika katika nafasi
hiyo kimataifa.
Drogba alipigia debe kumalizika kwa mgogoro wa kisiasa na pia
kuhimiza pande zilizozozana kupatana.
BBC/SWAHILI
P
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni