Jumanne, 28 Machi 2017

UZINDUZI WA KITAIFA WA TOVUTI ZA MIKOA NA HALMASHAURI


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika katika  Ukumbi wa HazinaMjini Dodoma 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene akizindua tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo  mjini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe. (Kushoto)  ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Mhe. Said Meck Sadick wakifuatilia uzinduzi huo.
 Msanii Mrisho Mpoto akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene,  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na viongozi mbalimbali katika Mikoa na Halmashauri wakifuatilia uzinduzi wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika  jana Mjini Dodoma katika Ukumbi wa Hazina. Tovuti hizo zinalenga katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa haraka ikiwa ni pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka.
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Mhe. Said Meck Sadick akiongea katika uzinduzi huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni