Jumanne, 28 Machi 2017

LIONEL MESSI APATA MAJANGA

Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA March 28 limetangaza taarifa ambazo haziwezi kuwa nzuri kwa mashabiki na wapenzi wa naodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ambaye pia anaichezea FC Barcelona ya Hispania.


FIFA leo wametangaza kumfungia mechi nne Lionel Messi kufuatia kosa alilolitenda March 24 wakati wa mchezo dhidi ya ChileMessi amefungiwa kutokana na utovu wa nidhamu wa kumtolea lugha isiyo ya kiungwana refa wa mchezo huo.
Adhabu hiyo ya Lionel Messi inaambatana na faini ya pound 8100, hivyo kufuatia adhabu hiyo Lionel Messi sasa ameanza kuitumikia kwa kukosa game dhidi ya Bolivia leo iliyomalizika kwa Argentina kupoteza kwa goli 2-0.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni