Jumamosi, 17 Desemba 2016

ZULU ASHINDWA KUICHEZEA YANGA Vs JKT RUVU HANA KIBALI CHA KUFANYA KAZI NCHINI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

KIUNGO mpya wa Yanga, Justin Zulu ameondolewa ghafla katika kikosi cha Yanga kilichocheza na JKT Ruvu jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na kutopata kibali cha kufanya kazi nchini.

Mapema jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilionya mchezaji ambaye hatakuwa na kibaki cha kufanya kazi nchini kutoka Idara ya Uhamiaji hatacheza na Yanga inakuwa ya kwanza kukumbana na kibano hicho.

Yanga ilimenyana na JKT Ruvu  leo katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Awali, jina lake liliwekwa kwenye kikosi cha watakaoanzia benchi, lakini baadaye likaondolewa na kuwekwa jina la Said Juma ‘Makapu’.
Justin Zulu akiwa jukwaani

Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya JKT Ruvu sasa ni; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Simoni Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.

Katike benchi baada ya kuondolewa Zulu wanabaki Ally Mustafa ‘Barthez’, Hassan Kessy, Vincent Andrew, Obrey Chirwa, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’ na Geofrey Mwashiuya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni