Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii
Imeelezwa watoto wengi wa kike wanakosa muda wa kuzungumza na wazazi wao wa kiume juu ya masuala ya mabadiliko ya kimaumbile hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kwa watoto wa kike kujiingiza katika vishawishi mbalimbali.
Hayo yamesemwa na mkuunzi wa masuala ya kijinsi na jinsia kutoka tasisi isiyo ya kiserikali ya TGNP,Liliani Liundi katika warsha kuhusu kupigania usawa wa kijinsia kwa mtoto wa kike haswa katika kuangalia vipaumbele vya sekta ya Afya ,Maji , Elimu , Kilimo na Viwanda.
"Ifike muda sasa kwa wazazi wa kiume waanze kuanza kuzungumza na watoto wao juu ya masuala ya mabadiliko ya kimaumbile na kuweka bajeti kwa watoto wa kike katika familia na kutenga vyombo maalum vya kuhifadhia taka zinazotokana na matumizi ya vifaa vya kimaumbile ya mtoto wa kike kisha kuzichoma"amesema.Liliani Lihundi.
Kwa upande wake muwezashaji mwingine kutoka TGNP ,Deo Temba amesema kuwa ukosefu wa elimu salama ya uzazi wa mpango umechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mimba za utoto kwa watoto waliopo chini ya miaka 18 nchini hali inayohatarisha kuwepo na nguvu kazi ya usawa kwa vijana wetu.
Katika mjadala huo amesema ni vyema jamii ikajipanga upya na kufikiria kuboresha mfumo wa utoaji elimu ya afya ya uzazi katika jamii na kuvunja mfumo dume unaobebwa na mila na desturi hasa kwa kutumia sanaa na kutumia vyombo mbalimbali vya habari.
Mkufunzi wa masuala ya kijinsia kutoka TGNP, Lilian Liundi akizungumza na wadau walioshiriki katika warsha hiyo.
Muwezeshaji kutoka TGNP, Deo Temba akitoa mada katika warsha hiyo ya wadu wa sanaa na waandishi wa habari iliyofanyika ofisi za tasisi hiyo Mabibo.
Washiriki wa semina hiyo wakifatilia kwa makini mafunzo hayo.
Washiriki wakisikiliza kwa makini mafunzo hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni