Jumanne, 20 Desemba 2016

TANZANIA YAPOKEA MKOPO WA SH. BILIONI 360 WENYE MASHARTI NAFUU KUTOKA AFDB

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero wakisaini mikataba miwili ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya shilingi Bilioni 360 kwa ajili ya kuongeza Ufanisi wa Tanesco na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Wakulima nchini-TADB, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero(kulia), wakibadilishana mikataba ya Mkopo wa Sh. Bilioni 360, zitakazo kwenda katika Sekta ya Nishati ya Umeme na Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini-TADB, tukio lililofanyika makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dare salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa tatu kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero(wa pili kulia), wakisaini mikataba miwili yenye thamani ya Sh. Bilioni 360 kwa ajili ya kutunisha mfuko wa bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 na kuendeleza kilimo kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo-AFDB, huku wakishuhudiwa na Mafisa wa pande zote mbili. Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje Mamelta Mutagwaba na wa pili kushoto ni Naibu Kaibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Hamis Shaban, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia), akizungumza baada ya kusaini Mikataba miwili ya Mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya shilingi Bilioni 360, ambapo ameshauri fedha hizo zitumike kikamilifu katika maeneo husika ambayo ni Bajeti na kuendeleza kilimo. kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) akipiga makofi baada ya Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia), kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za maendeleo ya Uchumi hasa katika viwanda, baada ya kusaini mikataba miwili ya Sh. Bilioni 360, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni