Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, imempata Meya mpya na Naibu wake baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa madiwani wake Desemba 17, 2015. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeweza kuibuka na ushindi wa nafasi zote mbili.
Manispaa hiyo imefanya uchaguzi ikiwa ni baada ya kuundwa kwa wilaya mpya mbili ndani ya Jiji la Dar es salaam, ambazo ni Ubungo na Kigambo na kufanya jiji la Dar es Salaam kuwa na Manispaa tano zikiwepo zile za awali za Ilala, Temeke na Kinondoni.
Haya ndio matokeo ya kura hizo.
Matokeo ya Meya
Kura zilizopigwa- 15
Kura iliyoharibika- 1
Maabadi Suleiman Hoja (CCM-Pembamnazi)- 9
Celestine Maufi (CDM-Mjimwema)- 5
Matokeo ya Naibu Meya
Kura zilizopigwa- 15
Amin Sambo (CCM-Kibada)- 10
Ernest Mafimbo (CUF-Tungi)- 5.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni