Jumamosi, 17 Desemba 2016

BONDIA FRANCIS CHEKA ANAINGIA ULINGONI LEO DHIDI YA MPIGANAJI WA INDIA VIJENDER SINGH JIJINI NEW DELHI


Ni Mjini New Delhi bendera ya Tanzania kwa mara nyingine inapeperushwa katika michezo inapeperushwa na  Bondia  Francis Cheka ambaye anaingia ulingoni dhidi ya mpiganaji wa India Vijender Singh katik pambano la ubingwa la Super Middleweight .
Kwa mujibu wa msomaji wetu Khadija Deddah ambaye yuko nchini India, pambano hilo linatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa.
Francis Cheka ambaye ni bingwa wa zamani  anapambana na  Singh ambaye anatetea taji lake la WBO Asia Pacific super middleweight. Vijender ambaye alishinda taji hilo Julai mwaka huu kwa kumtandika bingwa wa zamani wa Ulaya Kerry Hope wa Australia mpaka sasa hajapoteza kitu ulingoni. 
Katika gemu hiyo ya raundi 10 Francis Cheka anatarajiwa kutumia uzoefu wake mkubwa kumtandika bingwa huyo na kumpokonya mkanda wake. 
Wakati wa  upimaji uzito jana Francis alisema kwamba atazungumza ulingoni wakati Vijender akisema kwamba mkanda hauendi kokote utabaki nchini India. Cheka mwenye umri wa miaka 34 ni veterani akiwa amepigana mara 43 na kushinda mara 32 zikiwamo TK 17. Mpambano wa Cheka na  Singh utatanguliwa na mapambano mengine matano ya kirafiki ya kimataifa.
 Watanzania (wanafunzi) walifika uwanjani kumshangiria Cheka
 Bango la pambano
 Uwanja wa pambano
 Kutoka kushoto ni  Naibu Balozi wa Tanzania nchini IndiA, Katibu wa Shirika la Kimataifa (AALCO) ambae ni Mtanzania, na Afisa wa Ubalozi
Wanafunzi wa Ki-Tanzania wapo uwanjani kumshangilia Cheka

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni