Jumatatu, 10 Agosti 2015

MAGUFULI AWASHUKURU WANA CCM WA MTWARA KWA KUMDHAMINI,WAMUHAKIKISHIA USHINDI WA KISHINDO

  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanachama na wafuasi wa CCM mkoa wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kumpokea,Dkt Magufuli aliwashukuru wanachama hao kwa kujitokeza kwa wingi na walimuahakikishia ushindi wa kishindo na wa mapema katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo baadae mwaka huu,pia amewata kuwa na umoja wa kushirikiana na kuweka kando tofauti zao kuhakikisha wanailetea CCM ushindi wa kishindo.
 Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Husnain Murji akiwahutubia wana CCM nje ya ofisi ya CCM Mtwara na kuwaambia kuwa ushindi kwa CCM utakuwa wa kishindo .
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani akihutubia wakazi wa Mtwara  ambapo alihakikisha kuwa Mtwara itaongoza katika kumpigia kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Wananchana na Wafuasi wa chama cha Mapinduzi (CCM),wakimshangilia  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli  alipokuwa akiwashukuru kwa kumpa udhamni na kujitokeza kwa wingi kumpokea,lakini pia alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwao na kuwaomba wajenge mshikamano na kuweka tofauti zao kando ili kukihakikishia ushindi chama cha CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo baadae mwaka huu.

 Mgombea mteule wa Urais kwa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara,Ndugu Shaibu Akwilombe mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Mtwara kuwashukuru Wanachama na wafuasi wa chama hicho kwa kujitokeza kwa wingi,na pia alitia saini vitabu vya wageni vya ofisi hiyo,kati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani pamoja na Naibu Waziri wa Fedha,ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba.
 Baadhi ya Wanachama na wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi ya za mkoa huo mjini Mtwara,kabla ya kumsikiliza mgombea Urais wa chama hicho Dkt John Pombe Magufuli,ambaye alifika ofisini hapo kusaini vitabu na pia kuwashukuru wanachama huo kumdhamini na kujitokeza kwa wingi kumpokea

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni