Alhamisi, 4 Juni 2015

ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR DK.ALI MOHAMED SHEIN- UJERUMANI


1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Maritim Hotel Bw.Wissmann katika Mji wa  Wurzburg Nchini Ujerumani jana alipowasili katika Mji huo akiwa katika ziara ya Kiserikali ambapo atahudhuria ufunguzi wa maonesho ya Muziki yanayojumuisha wasanii kutoka nchi za Afrika na Mabara mengine (kulia) Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Philip Marmo, [Picha na Ramadhan Othman.]
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Wazanzibari waliofika kuwapokea mara walipowasili Maritim Hotel katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani wakiwa katika ziara ya kiserikali pamoja na ujumbe wa Viongozi mbali mbali aliofuatana nao katika ziara hiyo inajumuisha na  maonesho ya Muzikiyanayojumuisha Wasanii mbali wa Nchi za Afrika na Mabara mengine ambayo hufanyika kila mwaka,
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Nd,Salum Khamis Nassor mara walipowasili Maritim Hotel katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) wakiwa katika ziara ya kiserikali Nchini humo,ambapo atatembelea Sehemu kadhaa za kihistoria na Kiuchumi
4
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi na Mmiliki wa Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar LTD Bw.Brian Thomson wakati alipowasiliMaritim Hotel akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) wakiwa katika ziara ya Kiserikali Nchini Ujerumani pamoja na Ujumbe waliofuatana nao,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni