Lowassa Aendelea Kupata Maelfu ya Wadhamini
Mikoa ya Katavi na Rukwa
Mpekuzi blog
Waziri mkuu wa zamani Mh. Edward Lowasa ameendelea na ziara yake ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Katavi na Rukwa na kupata maefu ya wadhamini na amewataka waananchi waliojiandikisha kutunza vizuri shahada zao kwani ndio tiketi ya kuwawezesha kufikia ndoto zao za kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Mh. Lowasa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda na kupata mapokezi kishindo na wadhamini zaidi ya elfu tatu aliwashukuru wote waliompokea na kuwataka kuendelea kuhamasishana kujiandikisha na baadaye kupiga kura muda ukifika.
Awali mwenyekiri wa CCM wa mkoa wa Katavi Bw Mselem Saidi Abdllah aliwataka wanaccm kote nchini kuwatendea haki wagombea wote wanaotafuta wadhamini kwani kwa vyovyote vile mmoja wao ndiye atakayekuwa kiongozi wao.
Lowasa ambaye pia jana alitembelea mkoa wa Rukwa na kupata wadhamini wengi, leo ataendelea kutafuta wadhamini katika mkoa wa Kagera.
Mpekuzi blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni