WAZIRI wa ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyela(CCM) amewapongeza wakazi wa kyela kwa ushirikiano.
Dk. Mwakyembe alitoa pongezi hizo kufuatia umati mkubwa wa Wananchi kujitokeza katika mazishi ya kaka yake
Christian Mwakyembe aliyefariki dunia akiwa anatibiwa nchini India na kuzikwa kijijini kwao Ikolo wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.
Akizungumza kwa niaba ya familia ya Mwakyembe, Dk. Mwakyembe alisema ushirikiano uliooneshwa na wananchi wa Kyela na Watanzania kwa ujumla tangu msiba ukiwa Dar es salaam, Mbeya mjini na hatimaye kijijini kwao ni mkubwa sana na unapaswa kupongezwa.
“Sisi kama familia hatuna cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu kwani mlikuwa nasi tangu
mliposikia Kaka yetu amefariki kule India alipoletwa Dar es salaam, kule Mbeya na hapa kijijini Kwetu tunashukuru sana” alisema Dk. Mwakyembe.
Hata hivyo shughuli za msiba huo zilibebwa na Chama cha waandishi wa habari za uwekezaji na utalii(TAJATI) chenye makao makuu jijini Mbeya kufuatia mmoja wa wafiwa ni mwanachama wa chama hicho.
Mwanachama huyo Felix Mwakyembe ambaye ni mdogo wa Marehemu alipongeza namna wanaTajati walivyoshiriki kwa asilimia kubwa katika shughuli za mazishi ikiwa ni kushusha mwili wa marehemu kwenye gari, kupeleka ndani kuutoa nje wakati wa ibada na kuupeleka makaburini kasha kushusha kaburini na kuzika.
“ Niwashukuru sana wenzangu kwa sapoti mliyonipa sina cha zaidi zaidi ya kuwashukuru moyo mlioonesha ni mkubwa sana” alisema Felix Mwakyembe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni