Alhamisi, 14 Mei 2015

Utafiti wa TEDRO Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Lowassa Anaongoza kwa Kukubalika akifuatiwa na Mwigulu Nchemba.....Dr. Slaa Yupo Nafasi ya Tatu

Utafiti wa TEDRO Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Lowassa Anaongoza kwa Kukubalika akifuatiwa na Mwigulu Nchemba.....Dr. Slaa Yupo Nafasi ya Tatu

@Mpekuzi blog

Kutokana na kero zinazowakumbuka wananchi kuhusu suala la elimu, maji na afya taasisi ya utafiti wa Maendeleo ya Elimu nchini Tanzania (TEDRO) imetoa ripoti ya tafiti yake iliyofanya mikoa mbali hapa nchini juu ya Viongozi wanaoaminiwa na wananchi kuwa wakikamata nchi wanaweza kumaliza matatizo hayo.
 
Kutokana na ripoti hiyo ya Taasisi ya utafiti (TEDRO) inaonesha kuwa endapo uchaguzi ukifanyika leo chini Tanzania, Mh. Edward  Lowassa, Mwigulu Nchemba na  Dr. Slaa ndio wenye nafasi kubwa ya Kushinda nafasi hiyo.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa TEDRO Joseph Kateli amesema Utafiti huo umefanyika kwa kuzungumza na Watanzania kadha wakadha mikoa tofauti ya Tanzania na kila mmoja alikuwa na uhuru wa kumtaja kiongozi anayemtaka
  
Kura hizo ni kama ifuatavyo
1. Edward Lowassa 26%
2. Mwigulu Nchemba 23%
3. Dr. Wilbroad Slaa 22%
4. Ibrahim Lipumba 7%
5 Prof. Mark Mwandosya 6%
6. Mizengo Pinda 5%
7. John Magufuli 3.8%
8. Bernard Membe 3%
9. Fredrick Sumaye 2%
10. Steven Wassira 1.80%
  
Nini maoni yako juu ya utafiti huu?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni