Tutarajie kumuona Lupita kwenye hii movie nyingine kali Holywood !!
Lupita Nyong’o ni moja ya waigizaji wa kike wakubwa duniani.. Kenya inajivunia huyu staa wao, alianza kuonekana kwenye movie ya ‘12 Years A Slave’.. baada ya hapo milango ikafunguka upande wake, tukamuona tena kwenye movie ya Non-Stop.. Tayari ana Tuzo kubwa mikononi mwake na kazi ya movies inaendelea kama kawaida yani.
Mwaka jana kulikua na fununu kua staa huyo mpya wa hollywood ataigiza tena kwenye movie nyingine kubwa ya Hollywood movie series ‘Star Wars Episode VII – The Force Awakens‘ alafu baadae ikawa kimya.. kipya kwenye headlines ni kwamba rasmi kabisa taarifa imetolewa kwamba Lupita atakuwepo kwenye ‘Star Wars Episode VII – The Force Awakens’.
Movie itaachiwa cinema December 18 2015 ambapo Lupita amecheza kama “Maz Kanta”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni