Baadhi ya wadau walioshiriki kikao cha kwanza cha siku ya mtoto wa afrika katika Halmashauri ya Mji wa Njombe
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Wadau Mbalimbali Wameombwa Kuanza Kujitokeza Kuchangia Katika Maandalizi ya Kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika Hapo Juni 16 Mwaka Huu.
Wito Huo Umetolewa na Mratibu wa Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Hosea Yusto Wakati Akizungumza na Wadau Mbalimbali Mkoani Njombe Katika Kikao Cha Kwanza Cha Maandalizi ya Siku Hizo.
Bwana Yusto Amesema Kuwa Halmashauri ya Mji wa
Njombe Imepewa Kazi ya Kuandaa Maadimisho Hayo Kiwilaya Ambapo Yatafanyika Katika Mtaa wa Itulike Kata ya Ramadhani Kwenye Shule ya Msingi Itukike.
Amesema Kuwa Walemavu Hao Wanatakiwa Kukumbukwa Siku ya Mtoto wa Afrika Kwa Kuwanunulia Mahitaji Yao Muhimu Pamoaja na Kuwafanya Walemavu Hao Kuepukana na Suala la Walemavu Kuishi Kwa Kuomba Omba Mitaani na Kudharaulika Kila Siku.
Katika Hatua Nyingine Amesema Kuwa Maadhimisho Hayo Yamelenga Kuwasaidia Walemavu Hao Tofauti na Mwaka Jana Walitembelewa Watoto Yatima Katika Vituo Mbalimbali Huku Akiwataka Wa;lemavu Hao Kujiunga na Shirika la Walemavu Lilipo Njombe.
Hata Hivyo Ameitaka Jamii Kuacha Tabia ya Kuwaficha Walemavu Ndani na Badala Yake Wanashindwa Kufahamika Ili Waweze Kusaidiwa Ikiwa ni Pamoja na Jamii Kutambua Kuwa Suala la Kuyasaidia Makundi Hayo Siyo la Serikali Pekee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni