Ijumaa, 1 Mei 2015

RC NJOMBE AZINDUA RASMI TUZO YA TAALUMA YA MKUU WA MKOA.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi Akizindua Rasmi Tuzo ya Taaluma ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Wakati wa Kilele Cha Wiki ya Elimu Mkoani Njombe.
Miongoni mwa Pikipiki Nne zilizotolewa kwa shule Nne Bora Mkoani Njombe.

 
Na Gabriel Kilamlya, Njombe
 
Mkuu wa mkoa wa njombe dokta rehema nchimbi amepiga marufuku vyama vya siasa  mkoani njombe kujihusisha katika kusaidia kuchangia tuzo ya taalumu ya mkuu wa  mkoa wa njombe na badala yake wahusike wadau tofauti na vyama hivyo.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizindua rasmi tuzo ya taaluma ya mkuu wa mkoa  wa njombe yenye kaulimbiu isemayo  njombe namba moja inawezekana na kwamba  kuzinduliwa kwa tuzo hiyo iwe hachu ya kupandisha kiwango cha taaluma mkoani hapa.
Dokta nchimbi amesema kuwa lengo kuu la kuanzisha tuzo hiyo ni kutaka  kuwahimiza wadau wote wa elimu kuona umuhimu wa kusaidia sekta hiyo,kuwaongezea moyo wa uvumilivu na ukakamavu walimu katika ufundishaji pamoja na wanafunzi wenyewe.

Katika hatua ningine amewaagiza wakuu wa wilaya zote za mkoa wa njombe kuona namna ya kuanzisha tuzo hiyo kwa ngazi ya wilaya hadi ngazi ya chini kabisa na kwamba jitihada zaidi kupitia wadau hao zisaidie kukuza kiwango cha elimu hadi mkoa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mitihani mbalimbali.
Katika uzinduzi wa tuzo hiyo afisa elimu wa mkoa wa njombe said nyasiro amesema kuwa miongoni mwa sababu kubwa zinazoonekana kushusha kiwango cha elimu mkoani hapa ni pamoja na utoro kwa wanafunzi pamoja na kuchelewa kuripoti kwenye shule walizopangiwa kwani hadi kufikia mwezi machi mwaka huu.
Jumla ya wanafunzi 1454 ambao ni sawa na asilimi 12.7 walikuwa hawajaripoti shuleni.
Katika hatua nyingine shule ya msingi iduchi iliyopo katika halmashauri ya mji wa njombe kata ya luponde imeonekana kupanda kitaalamu kwa kiwango kikubwa kwani katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka jana shule hiyo imefikia nafasi ya 13 toka nafasi ya mwisho ya 77 kati ya shule zote 77 zilizopo katika Halmashauri hiyo. 
Hata hivyo shule hiyo imefanikiwa kutwaa tuzo mbalimbali ikiwemo pikipiki moja pamoja na shule nyingine tatu za msingi na sekondari kutoka katika wilaya zote za mkoani kupata tuzo.
Pamoja na mambo mengine lakini pia mkuu huyo wa mkoa ametoa zawadi ya kuku mmoja mmoja na mchele kilo mbili kwa madereva  boda boda 30 kutoka katika vituo mbalimbali ndani ya halmashauri ya mji wa njombe kutokana na umahili wao katika kuendesha vyombo hivyo kwa umakini mkubwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni