Picha tofauti zikionyesha wafanyabiashara mbalimbali wa maduka katika mkoa wa Njombe wakiwa wamekusanyika nje ya mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Njombe kusikiliza kesi ya Mexons Sanga mfanyabiashara maarufu mkoani Njombe.
Happy Mwasamili mke wa Mfanyabiashara maarufu mkoani Njombe Mexons Sanga (wa kwanza) akitoka nje ya mahakama ya hakimu mkazi Njombe baada ya kesi iliyokuwa ikimkabili yeye pamoja na mumewe kufutwa leo.
Mfanyabiashara Mexons Sanga (wa tatu kutoka kulia) akiongoza na wakili wake kutoka nje ya mahakama mara baada ya kufutwa kwa kesi yake leo
Wafanyabiashara mbalimbali wa mkoani Njombe wakiwa wamekusanyika katika ukumbi wa Turbo uliopo mjini Njombe kufanya kikao baada ya kutoka kusikiliza kesi katika mahakama ya hakimu mkazi Njombe.
Mexons Sanga akiingia kusikiliza kilichojiri katika kikao cha wafanyabiashara mbalimbali mkoani Njombe
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Njombe akizungumza na wafanyabiashara (hawapo pichani) katika ukumbi wa Turbo mjini Njombe baada ya kutoka mahakamani kusikiliza kesi iliyokuwa ikimkabili mfanyabishara Mexons Sanga leo.
Mfanyabiashara Mexons Sanga na mkewe Happy Mwasamili (mwenye koti la njano) wakiwasikiliza viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Njombe (hawapo pichani).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni