Mtoto mmoja wa miaka minane amesafirishwa hadi nchini Uhispania
kutoka Morroco akiwa ndani ya sanduku kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa
Uhispania.
Mvulana huyo kwa jina Abou alipatikana ndani ya sanduku hilo
lililokuwa limebebwa na msichana wa miaka 19 kuelekea Cueta,eneo lililo karibu
na taifa la Morrocco siku ya alhamisi.
Wakati polisi walipolifungua sanduku hilo, mvulana huyo alikuwa
katika hali mbaya sana.Mvulana huyo kutoka Ivory Coast sasa anahudumiwa na
mamlaka ya Cueta.
Gazeti la Uhispania El Paris liliripoti kwamba msichana huyo wa
miaka 19 hana uhusiano na mtoto huyo na kwamba alilipwa na babaake ili kubeba
sanduku hilo.
Babaake mtoto huyo anaishi katika visiwa vya Conary na kwamba
alitarajia kuonana na mwanawe kulingana na gazeti hilo.
Chombo cha habari cha Uhispania Efe kimesema kuwa babaake
mvulana huyo ambaye anajulikana kama Abou alisafiri hadi nchini Ivory Coast
kumchukua mwanawe baada ya kuhamia katika eneo la Gran Canaria mwaka 2013.
Babaake baadaye aliripotiwa kumlipa raia huyo wa Morocco ambaye
alimsafirisha mtoto huyo kupitia sanduku.
Msemaji wa polisi aliiambia Efe:''Alionekana kusita na kama
ambaye hakutaka kupitia mpakani''.
CREDIT: BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni