Alhamisi, 14 Mei 2015

''MAPINDUZI BURUNDI''



''MAPINDUZI BURUNDI''

Mshirikishe mwenzako
Mnamo 13 mwezi May jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.Rais Nkurunziza alidaiwa kurudi nchini Burundi kutoka Tanzania ,lakini imethibitishwa kuwa leo, alishindwa kufanya hivyo na kwamba yungali nchini Tanzania.
18.05pm-Wanajeshi watiifu
Wanajeshi watiifu wapiga doria Bujumbura
Makundi hasimu ya jeshi la Burundi yamekuwa yakipambana kukidhibiti chombo cha kitaifa cha habari RTBN ambacho kilizimwa kwa mda .Duru zimearifu kuwa kituo hicho cha habari kiko chini ya udhibiti wa vikosi vinavyomtii rais Pierre Nkurunziza.
17.53pm-Viongozi wajadili Burundi
Baraza la usalama la umoja wa Afrika laijadili Burundi kwa sasa
Baraza la usalama la umoja wa Afrika limetuma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter likisema kuwa wanachama wa baraza hilo kwa sasa wanaijadili.
17.00pm-Wanajeshi wapiga doria
Maafisa wa polisi wapiga doria Burundi
Maafisa wa polisi waliojihami katika mji mkuu wa Burundi,Bujumbura wanaonekana wakilinda vizuizi vya barabarani leo
16.50pm-Mkutano kuhusu Burundi waendelea.
Mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Afrika
Baraza la usalama la umoja wa Afrika kwa sasa linaijadili Burundi.
tweets: "Chini ya Uongozi wa balozi Amina Diallo wa Niger,ni mkutano wa 507.Baraza hilo linaangazia hali ilivyo Burundi
16.10pm-RNTB yarudisha matangazo
Kituo cha redio
Kituo cha redio cha Burundi RNTB kimerudi hewani,chini ya wanajeshi walio watiifu kwa rais Pierre Nkurunziza kulingana na duru kutoka kwa wanajeshi.Tumethibitisha kuwa kimeanza kurusha tena matangazo.
15.50pm-Nkurunziza asema yuko tayari kusamehe
Ris wa Burundi Pierre Nkurunziza
Shirika la habari la Reuters limenukuu baadhi ya mahojiano yaliofanywa na rais Nkurunziza na kituo cha habari cha RTNB mapema leo.
''Ninalishtumu kundi lililopanga mapinduzi'',alinukuliwa akisema.
''Nwashkuru wanajeshi wanaorudisha hali ya kawaida na namsamehe mwanajeshi yoyote ambaye yuko tayari kusalimu amri''.
Lakini baada ya mahojiano hayo kulikuwa na vita karibu na kituo hicho cha habari ambacho kwa sasa kimezimwa.
15.47pm-Ramani ya Burundi
Ramani ya Burundi
Ramani ya taifa la Burundi.
15.45pm-Mji wa Bujumbura
Burundi
Mji wa Burundi Bujumbura ulivyo kwa sasa
15.30pm-Vyombo vya habari vyazimwa
KItuo cha habari cha Isanganiro
Kituo cha habari cha Burundi Isanganiro kimesema kuwa kimefungwa na vituo vyengine vya kibinafsi .Kituo hicho ni miongoni mwa vile vilivyotangaza mapinduzi siku ya jumatano.
15.17pm-Kituo cha habari
Askari Burundi
Kituo cha habari cha Redio ya RTNB kimezimwa kufuatia mapigano makali karibu na afisi zake mjini Bujumbura.
15.01pm:Rais wa Burundi Ahojiwa
Wanajeshi nchini Burundi wakipiga doria
Kituo cha habari cha Burundi RTBN kimemhoji rais Pierre Nkurunziza kwa simu mwendo wa saa sita.Vita vimezuka karibu na afisi za kituo hicho cha habari.Jenerali anayeunga mkono jaribio hilo la mapinduzi amekiambia chombo cha habari cha AFP kwamba vitengo vinavyopigana kumpindua vimepata agizo la kukiteka kituo hicho habari cha RTNB kwa kuwa wana uwezo.
14.30pm:Makundi ya vijana waliojihami
Vijana Burundi
Kuna madai kwamba kundi la vijana linalunga mkono serikali limeshambulia kituo kimoja cha habari cha kibinafsi mjini Bujumbura.KUndi hilo linalojulikana kama Imbonerakure,baadhi ya watu wanaamini kwamba vijana hao wanatumiwa kama wapiganaji na kwamba huenda wamepewa silaha ili kuwatishia raia kabla ya uchaguzi.
13.45pm-Hali ni tete Burundi
Wanajeshi wa BUrundi
Hali bado ni tete nchini Burundi siku moja tu baada ya jenerali mmoja wa jeshi kujaribu kutekeleza mapinduzi .Barabara nyingi zimeendelea kuwa bila watu kwa kipindi kirefu cha alfajiri huku wengi wakisalia ndani ya majumba yao wakihofia usalama kulingana na mwanahabari wetu Ruth Nesoba.
13:30pm-Ukabila
Kiongozi wa jeshi aliyetangaza mapinduzi
Tofauti zilizopo katika jeshi la Burundi kufuatia jaribio la mapinduzi hazionekani kuwa katika misingi ya kikabila ,mkuu wa majeshi ambaye ni mtiifu kwa rais Nkurunziza pamoja na jenerali wa majeshi aliyetangaza mapinduzi hayo ni wa kabila la Hutu.Makundi hayo yanaonekana kugawanyika kati ya wale wanaoamini rais Nkurunziza alikiuka makubaliano ya amani yaliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa kutaka kuongoza kwa muhula wa tatu na wale wanaosalia kuwa watiifu kwake
12:05pm-Wanajeshi watiifu
Mj wa Burundi Bujumbura
Afisa mmoja wa kijeshi ameiambia BBC Afrique kwamba wanajeshi watiifu nchini Burundi wanadhibiti mji wa Bujumbura ,uwanja wa ndege,makao ya rais pamoja na vituo vya redio na runinga.
12:00pm-Milio ya Risasi
Wanajeshi wa Burundi
Makundi hasimu ya askari yanakabiliana katikati mwa mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni