Majirani wamechukizwa na manyanyaso anayofanyiwa Housegirl, wanataka bosi wake akamatwe !!
Leo Tena ya akina Geah Habib, Husna Abdul na Mussa Hassan ilikuwa hewani on #CloudsFM kuanzia saa 4 mpaka saa 7 mchana.. ilikupita? Niko nayo hapa, stori inahusu unyanyasaji wa msichana wa kazi Kitunda.
Mjumbe wa eneo hilo amesema alipata taarifa kwamba msichana huyo ananyanyaswa na kupigwa na mama ambaye ni bosi wake, akamfuata na kumpeleka Hospitali, majirani hawakuridhika wanataka mama huyo akashtakiwe kutokana na vitendo vya unyanyasaji ambavyo amekuwa akivifanya kwa sababu hiyo sio mara ya kwanza.
Polisi walifika kwenye nyumba ya mama huyo, lakini alijifungia ndani akagoma kabisa kufungua mlango.. Polisi wakaacha maagizo kwamba mume wake ampeleke mwanamke huyo kituoni ili akachukuliwe maelezo.
Majirani wamesema mama huyo amesingizia kwamba kinachofanya awe mkali na kumpiga msichana huyo ni ujauzito alionao, lakini sio kweli kwa sababu hii sio mara ya kwanza kuwapiga na kuwanyanyasa wasichana wake wa kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni