Ijumaa, 8 Mei 2015

Khadija Kopa: Viongozi wa taarabu wanyonyaji

SHARE THIS
TAGS
KopaNA THERESIA GASPER
MWIMBAJI wa muziki wa taarabu, Khadija Omari Kopa, ameweka wazi kwamba baadhi ya viongozi wa bendi za taarabu huwanyonya kimapato wasanii wao ndiyo maana wengi wao hawana afya nzuri.
Khadija Kopa alisema licha ya kutokuwa na afya nzuri, wengine hushindwa kujiendeleza kimuziki kutokana na namna wanavyobanwa na viongozi wao kwa kuwa wanahofia maendeleo ya wasanii wao yanaweza kusababisha wakahamia bendi nyingine.
“Viongozi wengi wananyonya wasanii wao hivyo wasipojishughulisha na kazi nyingine binafsi hawawezi kupata maendeleo, mimi bila kujishughulisha na kazi nyingine nisingekuwa hivi wala jina langu lisingekuwa kubwa hivi,” alifafanua
Kwa sasa malkia huyo wa mipasho anamiliki bendi yake binafsi anayoiita Kopa Kopa, ambayo hata hivyo anajipanga ili kuifanyia uzinduzi rasmi ili ianze kufanya maonyesho ndani na nje ya nchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni