Katika
ulimwengu ambao watu hutumika na utandawazi na si watu kuutumia utandawazi,
taarifa na habari ni kiungo muhimu sana katika maisha ya walimwengu. Ili kupata
habari za uhakika na kwa muda muafaka basi ni lazima utandawazi uifanye dunia
iwe kama kijiji. kwa maana ya kurahisisha mawasiliano baina viumbe waliomo
ndani, na hapa ndipo tunapata kujionea matumizi ya mtandao ‘internet’ kama
chanzo cha habari na kiungo cha mawasiliano.
Ili
kurahisisha mawasiliano baina ya walimwengu kumekua na uanzishaji wa blogu,
mitandao ya jamii na vitu mbalimbali katika mitandao ili kurahisha mawasiliano
na upatikanaji wa habari.
Suala
la mitandao lina msaada mkubwa sana katika jamii tofauti na kundi la watu
linavyochukulia. Mtandao unaweza ukatumika kujisomea na kupata maarifa mapya
kama si kuongeza, kujuana na watu, kufahamiana, kupata habari na kupata
kuwasiliana.
Hapo
mwanzo watu walikua wanapata mtandao kupitia kompyuta, ila sasa watu wanaweza
kupata huduma za mtandao kupitia simu, saa na vifaa vingine vya kielektronic.
Chachu
hii imeongeza ugunduzi na ubunifu wa vifaa vingine vipya ili kukuza matumizi ya
kimtandao na kurahisisha kazi kwa watumiaji.
Katika
matumizi ya mtandao, jamii na jamii zinazidiana kutokana na sababu zisizo
zuilika kwa mfano hali ya maisha ya jamii husika.
Wakati
dunia nzima ina idadi ya watu wapatao 7,182,406,565, ni watu 3,035,749,340
ambayo inatengeneza 42.3% tuh ndio wanaotumia huduma ya kimtandao. Hii
inaonesha ya kuwa kuna idadi kubwa ya watu hawatumii huduma hii kwa sababu
tofauti tofauti.
Lengo
la makala hii ni kuangalia nafasi ya nchi ya Tanzania katika matumizi ya
mtandao ukilinganisha na nchi zingine za Afrika. Kwa kifupi Tanzania tupo nyuma
sana katika matumizi ya mtandao,
wakati
inakadiriwa idadi ya watu kufikia 49,639,138 ikiwa na watumiaji wa mitandao
7,590,,794 ambao ni sawa sawa na asilimia 15.3 na 2.5 ikilinganishwa na idadi
yaw a Afrika kwa ujumla.Watumiaji wa facebook kwa Tanzania ni 705,460, takwimu
hii ni kwa makadirio ya mwaka 2015.
Kwa
takwimu hizo inaonesha wazi kuwa Tanzania iko nyuma ya nchi zingine za Africa
kwa kiasi kikubwa. Kwa kuanzia Tanzania iko nyuma ya Kenya na Uganda, huku
Kenya ikichukua asilimia 47.3 ya idadi yote ya wakenya ambayo ni 45,010,056.
Wakati huo huo wakenya 2,045,900 ndio watumiaji wa mtandao wa jamii wa facebook
huku wakiipiku Tanzania.
Kwa
upande mwengine nchi ya Uganda japo inalega lega katka kiwango ya watu
wanaotumia mtandao wa jamii, asilimia 18.2 ya watu wake wanatumia mtandao
katika maisha ya kila siku. Kiasi hichi ni kikubwa kulinganisha na 15.3 ya
Tanzania.
Kama
haitoshi nchi zingine zimeendelea kuiacha nyuma Tanzania katika matumizi ya
‘internet’ mtandao na yale ya facebook. Nchi ya Madagascar ina watumiaji wa
internent asilimia 74.7 ya watu wake wote, huku nchi ya pili ikiwa Mali yenye
asilimia 72.1. Misri ikiwa na asilimia 53.2, Gabon ikiwa na asilimia 39.3,
Mauritius ikiwa na asilimia 39.0, Nigeria ikiwa na asilimia 39.7, Afrika ya
kusini kwa 51.1 na Zimbabwe kwa 38.8.
Takwimu
hizi ni kwa nchi chache tu za Afrika ili kuonesha ni kwa kiasi gani tumeachwa
katika matumizi haya ya mtandao. Si vibaya sana kuachwa kimatumizi kwani siku
zote binadamu hatufanani, ila hili halituzuii kuuliza au kujiuliza kunani? Na
kipi chanzo cha mwamko mdogo wa matumizi ya mtandao?
Kwa
kifupi sababu ni nyingi na tofauti tofauti, kwanza uwezo wa baadhi ya watu
kununua na kugharamia vifaa au vyombo vinavyowezesha matumizi ya mtandao ni
mdogo. Vifaa kama simu bora na zenye uwezo, kompyuta za aina zote na vinginevyo
imekua changamoto sana kwa mwananchi wa kawaida wa Tanzania kuweza kununua.
Sababu
ya pili yaweza kuwa uwezo wa kutumia vifaa vya kimtandao nao ni tatizo kwa
baadhi ya watu. Watu wengi wanashindwa kutumia mitandao mbalimbali kwasababu
ule uwezo na ufahamu kuhusu mitandao ni tatizo.
Mtu
hajui A’B’C zozote zinazohusu mitandao. Sababu nyingine yaweza kuwa utayari wa
watu katika kutumia mitandao na mitandao ya jamii.
Unakuta
mtu ana kompyuta, simu na kadhalika lakini anatumia kwa matumizi mengine kama
kuangalia muvi, kucheza gemu, kupiga au kufanya kazi za ofisi na kushindwa
kujiongeza kwamba kuna matumizi zaidi ya hapo.
Sababu
zingine zinaweza kuwa ukosefu wa nishati ya umeme kwa baadhi ya maeneo nayo ni
chanzo cha kuzembea kwa ukuajiwa watumiaji wa mitandao na mitandao ya jamii.
Uzembe kwa baadhi ya watu, na vile vilemuundo wa majukumu na kazi tunazofanya
hautupi mwanya wa kuhitaji kutumia mitandao kwa muda flani.
Kufuatia
sheria mpya ya mitandao, nachelea kusema ya kwamba kiwango cha watumiaji
kitakua kwa kasi ndogo sana na wakati mwwingine kinaweza kupungua kutokana na
watu kushindwa kupata uhuru kama ilivyo sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni