Jumatano, 18 Machi 2015

MAMA MMOJA WA MTAA WA GWIVAHA ADAIWA KUTELEKEZA WATOTO WAKE WATATU KWA MUDA WA MWEZI MMOJA NJOMBE

Na Mwandishi Wetu, Njombe


Diwani Wa Viti Maalumu Angela Mwangeni Amewataka Wananchi Kuwafikisha Katika Ofisi Za Serikali Za Mitaa  Na Kuchukuliwa  Hatua Kali Za Kisheria Baadhi Ya Wazazi  Ambao Wamekuwa Wakitelekeza Watoto Wao  Kwa Kushindwa Kuwapatia Huduma Muhimu  Ikiwemo Malazi,Chakula Na Elimu   Ikiwa Wanauwezo Mzuri Wa Kuwasaidia.

Kauli  Hiyo  Imetolewa Kufuatia Kuwepo Kwa Baadhi Ya Wazazi Ambao Wamebainika Kutelekeza Watoto Wao  Na Kwenda Kufanya Biashara Zao Nje Na Mazingira Ya Watoto  Ambapo Hali Hiyo Imebainika Katika Mtaa Wa Gwivaha Na Kutaka Wananchi Kuwa Wawazi Kutoa Taarifa Kwa Viongozi Wao Watakapo Baini  Baadhi Ya Wazazi Wametelekeza Watoto Wao.

Diwani Mwangeni Ametoa Kauli Hiyo Kufuatia Kumbaini Mama Mmoja Mkazi Wa Mtaa Wa Gwivaha Velonica Ilomo  Kuwatelekeza Watoto Wake Kwa Takribani Siku 30   Wanaosoma Darasa La Pili Na La Nne Katika Shule Ya Msingi  Luhuji  Ambao Mmoja Anaumri Wa Miaka Saba Na Mwingine Miaka 11 Wakiwa Wanajipikia Wenyewe.

 Bi. Mwangeni Amewaomba Idara Ya Maendeleo  Na Ustawi Wa Jamii Kutoa Elimu Kwa Wananchi Kupitia Radio Ili Wananchi Waweze Kufahamu Kanuni Na Sheria Za Kuwalea Watoto Na Adhabu Zitakazostahili Kuchukuliwa Kwa Mzazi Atakaye Kiuka Taratibu Za  Malezi Kwa Watoto.

Akizungumza  Kaimu Afisa Mtendaji Wa Mtaa Wa Gwivaha  Augustine Samson  Amesema Kuwa Serikali Ya Mtaa Wa Gwivaha Imeweza Kubaini Kuwepo Kwa Tatizo Hilo Baada Ya Kutebelea  Kaya Mbalimbali  Za Mtaa Huo  Ili Kubaini Changamoto  Zinazowakabili Ambapo Kutokana Na Kuwakuta Watoto Hao Wamepeleka Taarifa Hizo Kwa Afisa Ustawi Wa Jamii Na Dawati La Jinsia Juu Ya Kutelekezwa Kwa Watoto Hao.

Kwa Upande Wake Mama Wa Watoto Watatu Mmoja Akiwa Ni Wa Kaka Yake Waliotelekezwa Kwenye Mtaa Huo Katika Eneo La Mahakama Ya Mwanzo Bi.Velonica Ilomo Amekanusha  Kutelekeza Watoto Hao Kwa Takribani Siku 30  Ambapo Amekili  Kuwaacha Watoto Hao Kwa Muda Wa Siku Mbili  Ambapo  Kibiashara Amesema Anafanyia Kata Ya Lugenge Ambako Anauza Grosari Huku Akisema Alikuwa Anamuuguza Mmewe Katika Hospitali Ya Ikonda.

Kwa Upande Wao Majirani Wa Mama Huyo Wamesema Kuwa Mama Huyo Anatakribani Muda Wa Siku  14 Tangu Alipo Kuwa Ameondoka Bila Kuwaaga  Ambapo Tabia Kama Hiyo Imejengeka Kwa Mama Huyo Ya Kuwaacha Watoto  Hao  Wakiendesha Maisha Ya Nyumbani Wenyewe Kwa Kujipikia Chakula Na Kufua Nguo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni