Alhamisi, 12 Machi 2015

Kipigo cha Simba chamrejesha darasani Pluijm


Kocha Pluijm


Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, Pluijm ameandaa programu inayomtaka kila mchezaji wa timu hiyo kuanzia kipa hadi mshambuliaji wa mwisho, kupiga pasi sahihi kwa mtu aliye kwenye nafasi, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi kwa wachezaji wake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu.

Wachezaji Ally Mustapha, Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Kpah Sherman, Juma Abdul na Mrisho Ngassa walikuwa kivutio kwenye programu hiyo juzi kutokana na uhodari wao wa kupokea mpira na kupiga pasi kwa walengwa.
Kitu kingine ambacho Pluijm anakijenga kwa wachezaji wake ni umiliki wa mpira, ambapo sasa amewataka kuwa na uhuru pindi wanapokuwa na mpira mguuni na kuutafuta kwa haraka pindi wanapoupoteza kwa adui.
“Usikimbie na mpira mguuni. Mimi nataka kuona mchezaji anaonyesha ubunifu wake pale anapokokota mpira. Ubunifu unasaidia kumjengea hofu mpinzani wako pale anapokuzuia,” alisikika Pluijm akiwasisitiza wachezaji wake kwenye mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salam.
Pluijm pia, juzi alimfanyisha mazoezi ya peke yake kiungo Mbrazili Andrey Coutinho, ambaye alikosa mechi mbili zilizopita za timu hiyo kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Mbeya City mjini Mbeya.
Yanga imeamua kufanyia mazoezi yake Uwanja wa Taifa ili kujiandaa na mechi yake ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Platinum ya Zimbabwe.
Katika mazoezi ya juzi jioni, wachezaji Simon Msuva, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Danny Mrwanda walikosekana kutokana na sababu mbalimbali kama ilivyothibitishwa na meneja wa timu hiyo, Hafidh Salehe.
Cannavaro bado anauguza jeraha lake la jicho aliloshonwa nyuzi nne, Msuva anaumwa tumbo wakati Mrwanda alikuwa na udhuru.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni