Jumapili, 29 Machi 2015

HOSPITALI YA MT,MERU YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MASHUKA YA KUJIFUNIKIA WAGONJWA

3Mwenyekiti wa kikundi cha Upendo Family Group ,Faustine Mwanadago (kushoto)akimkabidhi msaada wa katoni ya maji muuguzi mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru,Sifael Masawe jana kikundi hicho kilipofanya ziara ya kutembelea wagonjwa hospitalini hapo,jumla ya mashuka 300 na maji katoni 10 zenye thamani ya zaidi ya sh,2 milioni zilikabidhiwa ,anayeshuhudia pembeni ni makamu mwenyekiti wa kikundi hicho,Jasmine Kiure(Habari Picha na moses mashalla wa jamiiblog.co.tz/)
1Mwenyekiti wa kikundi cha Upendo Family Group ,Faustine Mwanadago (kushoto)akimkabidhi msaada wa mashuka na maji muuguzi mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru,Sifael Masawe jana kikundi hicho kilipofanya ziara ya kutembelea wagonjwa hospitalini hapo,jumla ya mashuka 300 na maji katoni 10 zenye thamani ya zaidi ya sh,2 milioni zilikabidhiwa ,anayeshuhudia pembeni ni makamu mwenyekiti wa kikundi hicho,Jasmine Kiure.

Hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mashuka ya kujifunikia kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali   waliolazwa hospitalini  hapo hali ambayo imepelekea baadhi ya wagonjwa hao kulala bila kujifunika nyakati za usiku.

Kwa sasa hospitali hiyo ina jumla ya vitanda 500 na mashuka 300 wakati wastani wa kitanda kimoja kinatakiwa kuwa na  mashuka 8.

Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada wa jumla ya mashuka 100 na katoni kumi za maji kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo,muuguzi mfawidhi wa hospitali hiyo,Sifael Masawe alisema kuwa tatizo la uhaba wa fedha kutoka serikali kuu limechangia kukosekana kwa huduma mbalimbali hospitalini hapo yakiwemo mashuka.

Alisema kuwa  kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa hushindwa kujifunika mashuka nyakati za usiku  kutokana na uhaba wa mashuka hayo na kuwataka wadau mbalimbali mkoani Arusha kujitokeza kuokoa hali hiyo.

Akikabidhi misaada ya mashuka na maji kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika wodi wa akina mama hospitalini hapo ,mwenyekiti wa kikundi cha Upendo Family,Faustine Mwandago alisema kwamba misaada hiyo imegharimu kiasi cha zaidi ya sh,2 milioni.

Mwandago,alisema kuwa lengo la kukabidhi misaada hiyo ni kuonyesha upendo kwa watu wenye mahitaji mbalimbali sanjari na  kulienzi jina la kikundi chao kwa vitendo huku akiwataka wadau wengine kuwaunga mkono.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni