Tunafuatilia kwa karibu taarifa ya ajali mbaya sana ambayo imetokea eneo la Changalawe, Mafinga, mkoani Iringa basi la Majinja toka likitokea Mbeya kwenda Dar es salaam limeangukiwa na kontena na taarifa zisizo rasmi zinasema abiria wengi wamepoteza maisha yao.
Habari hizo pia zinasema hadi sasa kuna maiti 36 hospitalini na ambao wanatibiwa majeraha wodini ni wanne. Tunaendelea kufuatilia.
Taarifa ambayo kwanza ilianza kuenea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ajali ya basi la abiria na lori la mizigo, kipindi cha Leo Tena Clouds FM wameongea na mashuhuda kutoka eneo la Changarawe, Iringa ambapo wamesema ni kweli ajali hiyo imetokea na kuna idadi kubwa ya watu ambao wamefariki.
Mashuhuda wamesema basi la Majinja lilitokea Mbeya kuja Dar es Salaam limegongana na lori la mizigo katika eneo hilo, abiria waliofariki ni wengi japo idadi kamili haijafahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, kwa sasa yuko njiani kuelekea eneo la tukio ili kuona mazingira ya ajali na kutoa taarifa kamili kuhusu ajali hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni