Alhamisi, 8 Januari 2015

MAKALA YA SHERIA: JIFUNZE NAMNA YA KUANDIKA MKATABA KISHERIA UNAPOUZA AU KUNUNUA


Na  Bashir   Yakub
Katika shughuli zetu za kuuza na kununua  ambazo tunazifanya kila siku mikataba ya maandishi  ni jambo ambalo wengi tunakutana nalo. Mikataba hii iwe rasmi au isiwe rasmi suala la msingi ni kuwa  huwa tunaifanya. Aidha wakati mwingine si  wote wenye kuhusisha suala la mikataba ya maandishi  katika makubaliano yaombalimbali  na hii hutokana na  sababu mbalimbali ikiwemo ya kuaminiana. 
Kuhusu kuaminiana niseme jambo moja tu kuwa suala la mikataba ni muhimusana  hata kana  mwenzako unamuamini kwa kiwango cha juu kabisa( highest degree of trust). Nathubutu kusema kuwa hata awe mzazi wako kama kuna jambo la msingi mmelifanya  ni vema kukawapo mkataba wa maandishi.  
Nasema hivi kwakuwa kwa uzoefu wangu wa mambo haya  mara nyingi mgogoro hautokani na waliouziana  au kukubaliana isipokuwa mgogoro unakuja kuanzishwa na walio nyuma ya hao.  Kwa mfano baba anaweza kumpa mwanae kiwanja   na wasifanye  mkataba wowote wa maandishi kwa kuwa wanaaminiana. 
 Hiyo ikaenda kwa miaka kadhaa ambapo baba akawa amefariki. Baaada ya hapo anaibuka mtu anasema mimi  ni mtoto wa  marehemu kwa hiyo nahitaji  kiasi kadhaa kutokamali hii. Hapa mgogoro si kati ya baba na mwana tena   isipokuwa ni kati ya mwana na mtu mwingine. Kama huna mkataba wowote wa maandishi  mpaka kesi hii kuisha waweza kuwa umepoteza kila kitu. 
Huu ni mfano tu katika kusisitiza kuwa mtu asiseme mi na  fulani tunaaminiana. Mgogoro sio lazima utokane na nyie wawili  isipokuwa walio nyuma yenu waweza kuanzisha mgogoro.

MADHARA   YA   KUTOFANYA  MKATABA  WA  KISHERIA .
Ni vema sana kujihadhari kwakuwa ukisikia neno  mgogoro ujue kuna mambo makubwa mawili. 
Kwanza gharama kubwa ni uwezekano wa kupoteza kabisa ilemali na haijalishi iwe uliinunua au ulipewa isipokuwa tu ukishakuwa na mgogoro upo katika hatari hiyo. Pia gharama ya pesa  kama kuwalipa wanasheria, gharama za uendeshaji kesi,  nauli  na matumizi mengineyo ambayo hujitokeza bila hata kutarajia. 
Pili kuna  gharama ya muda . Hii  huhusisha  kushinda mahakamani kila siku  na wote mwajua  mahakama zetu  zilivyo, kushinda vituo vya polisi huku shughuli zako za msingi za kila siku zikisimama. Pia hapa  kuna muda wa  kusubiri hukumu ambapo kesi yaweza kukaa mahakamani hata miaka  sita . Hakika unakuwa umesurubika(suffer) na  umepoteza mambo mengi katika kushughulikia jambo hili.

NAIBU WAZIRI WA MIUNDO MBINU ISSA GAVU AFUNGUA MTAMBO WA KUSAFISHIA MAJI UZING'AMBWA.

 -Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (Gavu)akifungua kitambaa kama ishara ya Ufunguzi wa mtambo wa kubadilishia maji kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama huko Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (Gavu)akikinga Maji yaliobadilishwa kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama baada ya kufungua huko Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Wananchi mbalimbali wakinywa maji yaliobadilishwa kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama baada ya kufunguliwa huko Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (Gavu)akitoa hotuba wakati alipofungua mtambo wa kubadilishia maji kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.kulia yake nimuakilishi wa Taasisi ya Mork Water Solution ya Ujarumani Mikalen na kushoto yake ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Idriss Muhsin Hijja.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

FIVE NEW YEAR CAR RESOLUTIONS

 Save hundreds of bucks on car maintenance costs with these 2015 car resolutions,Advices Carmudi Tanzania.

January 2015, Dar es Salaam, Tanzania –  As we welcome the year 2015, it is, time for us to reflect on the car resolutions most of us never kept. Car owners set goals but often neglect getting maintenance on their cars to keep them in top shape and bring their cars in only when repairs are needed. Carmudi, the fastest way to buy and sell cars online shares with you some easy-to-keep 2015 car resolutions that’ll save you plenty of bucks down the road in the upcoming year.

Resolution 1. Carry out two check ups per year.
Are you confident that your car fluids, battery, brake system, steering and suspension are up to scratch? Think again! Unless you have scheduled two car check ups per year with an expert engineer, you cannot be sure. Only trusted experts can identify the smallest of problems and thus help you save on your maintenance costs in the longer term. If there is a problem, it will be picked up early on, and thus prevent it from turning into a more costly repair job. And when it comes to selling your vehicle, potential buyers will be very impressed both with the condition of your car and the maintenance documents that you can produce at the time of the sale. So get ready to cash in more from your car.
Result: Higher resale value, plus save up to 320,000 TZS on breakdown costs!

Resolution 2.  Avoid aggressive driving, be smart.
Are you an adrenaline-seeking, pedal-to-the-metal kind of driver? If so, then this resolution will surely be difficult to stick with. But it’s not impossible, and the savings will be well worth it. Stop the high speed driving, avoid quick starts and hard braking. Drive smart and increase your fuel efficiency by up to 40 per cent. Yes, 40 per cent! You can even further reduce your fuel costs by driving at the optimal fuel saver speed of between 50 and 60 Miles per hour.
Result: Increase your fuel efficiency by up to 40 per cent.

Resolution 3. Maintain proper tire inflation.
Over inflated tires coupled by poor road conditions - potholes, rocky roads etc, can lead to rapid wear and tear and even punctured tires. If you want to get the best performance out of your tires, then you must keep your tire inflation at optimal levels. How? Check the information provided by your tire manufacturer. Keep in mind that under inflated tires can reduce fuel efficiency by up to 15 per cent, reduce your tire life and can lead to maneuverability problems which can cause accidents.  
Result: Save on tire costs, fuel costs by up to 4 per cent, avoid risk of accidents and repair costs.

Resolution 4.  Keep up with fluid changes.
Place great importance on oil and transmission fluids, making sure to carry out regular fluid changes. Why? It will help to ensure the brakes and clutch system is well maintained. If you Ignore these details, you might eventually have to replace your brakes and clutch system. This can be rather expensive and time consuming. Replacing brakes can costs up to 600,000 TZS, and repairing clutch system can cost up to 2000,000 TZS.
Result: Avoid replacing the brake and clutch system - save more than 160,000 TZS

Resolution 5.  Keep your car clean.
Trash or mess can become a hiding place for problem spots and stains. So, keep your car clean and make use of your car care kit to remove spots or stains before they get out of hand. You will be surprised to know that dirt and grime can be very harsh on your vehicle, especially for the interior of your car. Investing in a good quality car mat and vacuuming it on a regular basis can fetch you good long-term returns.

Result: Save up to 5000,000 TZS to replace the entire interior of your car


AIRTEL KUZINDUA AIRTEL UNI 255 J-MOSI MAALUM KWA VYUO VIKUU DAR ES SALAAM


Afisa Masoko wa Airtel Henrick Bruno akionyesha moja kati ya vocha za Airtel UNI255 maalum kwa vyuo vikuu nchini tayari kwa uzinduzi jumamosi hii.
Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando amesema “Airtel Uni 255 ni huduma pekee yakibunifu toka Airtel Maalum kwa wanafunzi wa vyuo yenye kuwapa unafuu wa kuwasiliana wawapo chuoni, sasa wanafunzi wote wa chuo wanapotaka kupata nyongeza ya vile wanavyosoma kwenye mtandao huduma  hiii  ndio jibu sahihi kwao kutokana na unafuu wake kwenye inteneti

 ·                Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole kupamba uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UDSM
                                                                                                             
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imebainisha kuwa mwishoni mwa wiki hii itazindua rasmi huduma mpya maalum kwa ajili ya kutoa huduma nafuu za mawasiliano kwa wanafunzi walioko vyuoni katika chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM ambapo hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama Airtel UNI 255 kwa vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam itafanyika katika viwanja vya Mabibo hostel

Akiongea kuhusiana na uzinduzi wa huduma hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando amesema “Airtel Uni 255 ni huduma pekee yakibunifu toka Airtel Maalum kwa wanafunzi wa vyuo yenye kuwapa unafuu wa kuwasiliana wawapo chuoni, sasa wanafunzi wote wa chuo wanapotaka kupata nyongeza ya vile wanavyosoma kwenye mtandao huduma  hiii  ndio jibu sahihi kwao kutokana na unafuu wake kwenye inteneti, kupiga simu na hata sms. Huduma hii tayari tumeshaizindua kwa vyuo vikuu vingine vya Dodoma, Mbeya, Iringa, Mwanza na imeonyesha mafanikio makubwa sana kwa watumiaji wakiwemo wanafunzi na wale wote wanaotumia huduma hii maeneo ya vyuo”

“Airtel tumeona ni vyema tuizindua hapa katika vyuo vya Dar es salaam wiki hii siku ya Jumamosi pale mabibo hostel ambapo mbali na uzinduzi kutakuwa na tamasha kubwa litakalopambwa na watoa burudani nguli akiwemo Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole pmaoja na DJ maarufu jiji Dj Zero aliongeza kusema Mmbando

Nae meneja wa huduma hiyo ya UNI 255 Anethy Muga alisema “Airtel tumeoana hii ni huduma maalum kwa wanafunzi na ndio maana tukaona ni vyema kuizindulia katika Hostel zao pale mabibo ambapo tunaamini wanafunzi wengi wa chuo kikuu hapa jijini wanaifahamu na wanaishi mabibo hivyo wanakaribishwa katika uzinduzi huo ambapo kiingilo chake ni BURE”

Burudani zitakuwa zakutosha kupitia Airtel UNI 255  siku hiyo

Kampuni ya simu za mkononi ya airtel ilianzisha huduma ya UNI255 ili kuendana sambamba na mkakati wao wa kusaidia vyuo vikuu nchini kutumia ipasavyo huduma za mtandao ili kuboresha sekta ya elimu kwa lengo la kusaidia wateja wake walioko vyuoni kufikia malengo yao.


BONGO MOVIE KUPAMBA UZINDUZI WA KITABU CHA MAREHEMU KANUMBA LANDMARK HOTEL


 

UZINDUZI wa kitabu cha msanii wa filamu hayati Steven Kanumba unatarajia kuandika historia kufuatia maandalizi yaliyopangwa anasema mratibu wa tamasha hilo Mohamed Mwikongi ‘Frank’ amesema kuwa kutakuwa na mambo muhimu sana kwa ajili ya kumuenzi msanii huyo ambaye aliitangaza Tanzania kimataifa.

“Tumepanga kufanya mambo makubwa kwa ajili ya mwenzetu na tunataka ijengeke tabia ya kuenzi wasanii mbalimbali, pesa za uzinduzi wa kitabu hiki utafungua Kanumba Foundation kwa ajili ya kusaidia wanawake wajane na watoto yatima,”anasema Frank.

Frank anawakaribisha wadau wa Kanumba kwa kufika na kujione kazi za marehemu Kanumba na kuoshuhudia wimbo maalumu wa Marehemu Kanumba utakaoimbwa na mwanamuziki nyota Christian Bella kwa ajili ya tukio maalum .
                                         
Kitabu cha historia ya maisha ya mwigizaji nyota Swahilihood Hayati Steven Kanumba kinatarajiwa kuzinduliwa tarehe 10 January 2014 katika ukumbi wa Landmark Ubungo, uzinduzi huo utaambatana na maonyesho ya kazi za marehemu Kanumba alizowahi kushiriki na kuzifanya.

Mama yake mzazi akiongea na waandishi wa habari amewashukru wale wote ambao wamekuwa wakijaribu kufanya kazi ambazo kwa njia moja au nyingine zinamkumbuka mwanaye ambaye aling’ara katika tasnia ya filamu Swahilihood na kufanikiwa kutangaza Tanzania.

“Nawashukru sana watanzania na wale ambao si Watanzania wamekuwa faraja sana kwangu, hasa pale ambapo wamekuwa wakiona umuhimu wa kumuenzi Kanumba kwa njia tofauti tofauti, nawashukru sana, na najua kila mtu ana mchango mkubwa si rahisi kuwataja majina maana mpo wengi,”anasema mama Kanumba.

Kitabu hiki kinachohusu maisha ya Kanumba The Great Fallen Tree kimeandikwa na E. Emmanuel kutoka nchini Canada na kuhaririwa nchini Marekani na kufanyiwa uchapishaji nchini Kenya.

 
Uzinduzi wa kitabu utasindikizwa na Christian Bella na Bendi ya Malaika kiingilio ni Ths. 20,000/ na utapata kitabu kimoja bure  ukiingia tu mlangoni na kazi zote za Hayati Kanumba zitapatikana siku hiyo. USIKOSE TUKIO HILI LA AINA YAKE!

SERIKALI YATUMIA SHILINGI BILIONI 881 KATIKA MRADI WA REA AWAMU YA PILI

Na Greyson Mwase, Maswa.
Meneja Utaalamu Elekezi  kutoka  Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) Gissima Nyamohanga amesema kuwa serikali imetumia shilingi bilioni 881 katika mradi wa kusambaza umeme  vijijini  unaotekelezwa na  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili.

Nyamohanga aliyasema hayo kwenye  sherehe za uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini unaofadhiliwa na REA uliofanyika katika kata ya Shishiyu wilayani Maswa mkoani  Simiyu.

Alisema kuwa Mradi wa  REA  Awamu ya Pili  utaiwezesha  idadi ya  vijiji  vilivyounganishwa   na umeme 3734  kati ya vijiji 15,180 ambayo ni asilimia 24.6 kufikia vijiji 5,234 ambayo ni asilimia 34.5 ifikapo  mwezi Juni mwaka huu.

Aliongeza kuwa mradi wa REA Awamu ya Pili wa miaka miwili  ulioanza mwaka 2013, lengo lake lilikuwa  ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote Tanzania vinapatiwa umeme hivyo kuboresha maisha  ya wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Akielezea mchango wa mradi wa usambazaji wa umeme  vijijini  unaotekelezwa na  REA katika kuboresha maisha  ya wananchi Nyamohanga alisema kuwa awali wananchi  wote walikuwa wakilipa  shilingi  467,000 kama  gharama ya kuunganishiwa umeme ambayo ilikuwa ni kubwa na kupelekea  wananchi wachache wenye uwezo kuwa na  nishati ya  umeme huku  ikiacha kundi kubwa la wasio na uwezo kuishi  gizani.

Alisema kuwa katika Awamu ya Kwanza ya REA gharama za uunganishaji wa umeme  zilishuka kutoka  shilingi 467,000 hadi shilingi 177,000 na kuongeza kuwa katika kuhakikisha  kila mwananchi anakuwa na uwezo wa kuunganishiwa umeme  Serikali iliamua  kubeba  gharama zote kupitia REA Awamu ya Pili na wananchi kutakiwa kuchangia shilingi 27,000 tu kama kodi ya ongezeko (VAT).

Alieleza kuwa mara baada ya kumalizika  kwa Awamu ya Pili ya REA, viongozi wataainisha  vijiji ambavyo havijapata  umeme REA Awamu ya Pili, ambapo vitajumuishwa katika mradi wa REA Awamu ya Tatu.
Nyamohanga alieleza michango mingine kuwa ni  kufungua  fursa za ajira na uwekezaji kwa vijana wa kitanzania, ufaulu  kuongozeka kwa shule za sekondari na kuboreshwa kwa huduma za afya.

“Kwa mfano kwa shughuli za kiuchumi bei ya kusaga  debe la mahindi ilikuwa ni shilingi 1,000 itashuka  hadi shilingi  500 kutokana na kwamba mashine za kusaga zitakuwa zinatumia  umeme badala ya  dizeli kama zamani,” alisema Nyamohanga

Wakati huohuo Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya  Ziwa Mhandisi  Joyce Ngahyoma akielezea jinsi ya kuunganishwa na huduma ya umeme kwa wananchi wa vijiji  vilivyopitiwa na mradi wa REA  Awamu ya Pili alisema kuwa wananchi wanaoishi  mita 30 karibu na miundombinu ya umeme wataunganishiwa kwa shilingi  27,000 na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo kwa kuboresha makazi yao.

Alisema kwa wananchi wenye  nyumba zenye  vyumba viwili na vioski hawahitaji kufunga mfumo wa umeme kwenye nyumba zao (wiring) badala yake watashauriwa kununua kifaa maalumu kijulikanacho kama “UMETA” (Umeme Tayari) kinachoweza kutumika kama mfumo kwa kuwa na uwezo wa kuunganisha taa mbili na vifaa vingine  kama  vile jiko, friji na pasi.

Aliendelea kusema kuwa kifaa hicho kinachouzwa kwa gharama ya shilingi 37,000 kitakuwa ni mali ya mteja na endapo atahama makazi basi atakuwa huru kuhama pamoja na kifaa chake.

APPRECIATION IN LOVING MEMORY OF OUR BELOVED LEONARD MICHAEL MASHAKA

We the family of the late Leonard Michael Mashaka would like to offer our heartfelt gratitude and the deepest thanks to each and every individual who joined us, prayed, comforted, lent us a helping hand and shoulder to cry on at such a difficult and trying time, as we mourn our beloved Leonard Michael Mashaka, who was recalled to the LORD on the 23rdNovember, 2014 and laid to rest on the 26thNovember, 2014 at the Kinondoni Cemetery, Dar es Salaam.


We are immensely moved by the support shown by all of you and there are not enough words to begin to describe the gratitude that we feel. While it is not possible to thank each and every one by name, we would however, like to make specific mention  of the Principal Judge, Judges and staff of the High Court of Tanzania, Judge-in-Charge, Judges and staff of the High Court- Land Division, St. Martha Parish- Mikocheni, Mr & Mrs Golden Mlawi, Office of the IGP, CO Traffic Tanzania, UDSM Class of ’84 and ’85- FoL, St. Maximillian Kolbe Christian Community- Mikocheni, Queens VICOBA Group- Mikocheni, Teachers and Students of Form 5 & 6 – DIS, PCCB Staff, neighbours, friends, relatives and well-wishers.
We, the family of the late Leonard Michael Mashaka pray that you will accept our most sincere appreciation; it comes from the bottom of our hearts.

We will now and forever cherish the husband, father, brother and friend you were to us. May the LORD rest our beloved Leonard Michael Mashaka in eternal peace. AMEN.  

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA MRADI MKUBWA WA REA WA SHILINGI BILIONI 25.7 MKOANI SIMIYU

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo leo amezindua mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili, mkoani Simiyu ambapo vijiji 170 vimeunganishwa na mradi huo. 
Mwananchi kutoka katika kijiji cha Nyanguge kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu akiwasilisha hoja mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa kwanza kulia) mara Waziri alipotembelea kijiji hicho wakati akielekea kwenye uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili wenye thamani ya shilingi bilioni 25.7.
Mbunge wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda (kushoto) akitafsiri hotuba ya shukrani iliyotolewa kwa lugha ya kisukuma na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Shishiyu mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA Awamu ya Pili.


MKWARA WA MUUZA MAEMBE




TWAWEZA: MIJADALA YA WANANCHI KWA NGAZI ZA MIKOA



NEW YORK NEW YORK FEB 21 "THE BIGGEST BIRTHDAY PARTY TO START THE YEAR -ALL INVITED !


MHE RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA NA ZAIARA YAKE JIMBONI KWAKE CHALINZE

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi mjini Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, Pwani,  ambapo pamoja na kuwashuru kwa kumchagua, pia alisema atatumia unasheria wake kuwasaidia wakazi wa jimbo hilo wanaonyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuporwa ardhi.
 Ridhiwani akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Masoko mjini Chalinze
 Mkazi wa Chalinze, Bibi akitoa malalamiko yake mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete ya kudhulumiwa shamba lake na watu wasiojulikana.
 Mkazi wa Chalinze Methodius Kaijage, akiuliza swali kuhusu alama za x zilizowekwa kwenye nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa barabara ambazo alidai ni takribani miaka kumi imepita bila kupewa fidia hivyo kusababisha kukosa maendeleo.
 Sehemu ya wakazi wa Kata ya Bwilingu, wakiwa katika mkutano na mbunge wao mjini Chalinze. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

JANUARY SALSA NEWS

Happy New Year!

We hope you are all well rested from the holidays, it is time to return to Salsa!

Come and learn to dance, have fun, meet people and exercise :)

Thursdays at The Terrace @Slipway
Class 8pm until 9pm (10,000Tsh all levels)
Social dance from 9pm to 11pm

We are planning to have our monthly party in Zanzibar on Saturday 31st and have a weekend of workshops. 

MTOTO ALIBINO ANASAKWA MWANZA , WATU 15 MBARONI

Serikali mkoani Mwanza imesema hakuna kulala hadi mtoto Pendo Emmanuel (Albino) apatikane kufatia tukio la kutekwa kwaek na watu wasio julikana toka tarehe 27.12.2014 katika kijiji cha Ndami, Tarafa ya Mwamashimba Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza na kisha kutoweka naye kwenda kusiko julikana hadi sasa. 
Mkuu wa Mkoa wa MWanza Mhe Magesa Mulongo, akiongea na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo na kuwahusisha wananchi wakijiji hicho pamoja na uongozi wa Wilaya na Mkoa huku alitaka kujua hatua iliyofikiwa na wananchi hao katika kuwabaini waliofanya unyama huo. 
Mtoto Pendo alitekwa na watu wasiojulikana  usiku wa tarehe 27.12.2014 majira ya saa nne usiku akiwa amelala na wazazi wake nyumbani kwao na kisha watekaji kutoweka naye na kwenda kusiko julikana hadi sasa. Watu kumi na watano (15), wanahikiliwa na jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi. 
Akihutubia wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alisema ni tukio la kusikitisha kwani toka mwaka 2007 hakuna tukio la namna hiyo lililowahi kutokea katika Wilaya hiyo na tukio la mwisho lililotokea lilimkumba mwananchi wa Wilaya hiyo aliyekuwa amesafiri kwenda Mkoani Shinyanga kwa shughuli zake. 
Amesema kiburi walichonacho watekaji hakiwezi kuwa nje ya mipaka ya kijiji hicho cha Ndami bali mpango mzima unajulikana kwa wenyeji na ndio maana ilikuwa rahisi kufanya unyama huo. 
“Kiburi cha watekaji kimo humu humu haiwezekani mtu kutoka mbali aje atekeleze tukio hapa kijijini bila ya kuwa na wenyeji lazima kuna mtu au watu walioshirikiana na wahalifu hao”, alisema Mulongo na kuongeza “ kwa mazingira ya Nyumba ya kina Pendo ilipo kule hakuna sehemu ya kutokea na kama mliona pikipiki inaranda randa mchana,.. iweje mshindwe kuitilia shaka? Hapana, hii haikubaliki! mimi nimekuja kuwaambia nataka Pendo apatikane na sio vinginevyo, nawapa siku tano Ijumaa nitarudi hapa mniambie Pendo yuko wapi! Alisema mkuu huyo wa Mkoa akionesha kusononeshwa na tukio hilo. 
“Mbona mifugo inapoibwa inapatikana”? Aliwahoji viongozi wa sungu sungu na kusema haiingii akilini kusema wakati wa tukio la utekaji sungu sungu wote walikuwa wamekwenda kula chakula na ndipo kadhia hiyo ilipotokea
Mkuu wa mkoa alihoji kufatia kauli iliyotolewa na kiongozi wa sungusungu kuwa wakati wa tukio askari wote wa sungu sungu walikuwa wamekwenda kula majira ya saa tatu na tukio kutokea saa nne. 
MWENYEKITI WA ALBINO MWANZA. Awali akielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo, Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa Ngozi mkoani hapa Alfred Kapole, alisema inasikitisha kuona wanadamu wakiwauwa binadamu wenzao kama vile wanyama bila hata woga na vyombo vya maamuzi vikishindwa kutoa hukumu kwa wakati huku akielekeza lawama zake kwa mahakama na Mkemia Mkuu. 
“Mh. Mkuu wa mkoa inasikitisha kuona miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa mahakamani, ni kesi 3 tu ndizo zilizokwisha kutolewa hukumu” alisema Kapole, na kuongeza ingekuwa ni kesi ya wabunge wameshindana kwenye masuala ya uchaguzi ingekuwa imekwisha hukumiwa lakini kwa kuwa ni mlemavu wa ngozi, basi kupuuzia kumekuwa kwingi mno",Alisema kapole. 
Akinukuu maneno kutoka katika kitabu cha Biblia, Kapole alisema hata kama hukumu zitashindwa kutolewa na wanadamu hapa Duniani, naamini Mungu wa Mbinguni kuna siku haki itatendeka kwa kuwa “Kitabu cha Mika 3.3-7 kinaeleza juu ya hukumu watakayo ipata watu walao nyama za watu bila woga. 
Kesi zinaendeshwa Polisi wanajitaihidi sana lakini mkemia watendaji wa ofisi ya mkemia mkuu wanatuhujumu kwa kuita nywele zetu albino ni za Midoli, aling’aka Kapole wakati akielezea kusikitishwa na ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali pindi inapo pelekewa Nywele. 
Mwenyekiti Kapole pia aliomba kwa yeyote aliye na Mtoto huyo kumrejesha na kama wamemdhuru basi warejeshe hata mwili wake ili matanga yaweze kufanyika, akatumia fursa hiyo kumomba Rais wale wote waliohukumiwa kunyongwa wanyongwe ili kuepusha kuendelea kula chakula cha serikali bure. RC ITIKADI KATIKA KAZI. Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa aliwataka wanachi kuweka mbali itikadi zao za namna yoyote na kufanya kila linalowezekana ili kufanikisha zoezi zima la kuwasaka walio husika na utekaji wa mtoto Pendo Emmanuel, ambao unasimuliwa kuleta siamanzi kubwa ndani ya jamii ya wana Kwimba na watanzania lakini pia kuchafua taswira ya nchi mbele ya mataifa mengine ya Dunia . Huku akiwaonya watu wa haki za binadamu kuacha kupaza sauti za kuwatetea wahalifu. Tanzania inatajwa kuwa kinara cha ukatili huo tangu mauwaji hayo yalipo zuka mwanzoni mwa miaka ya 2006/2007. 
TAKWIMU ZA KIMATAIFA. 
Kwa Mujibu wa takwimu za kimataifa zinaonesha ni asilimia 2% tu ya watu ambao huzaliwa na ulemavu wa ngozi ndio hufikia na kusherekea miaka 40 ya kuzaliwa kwao, huku pia takwimu zikionesha katika nchi za Afrika mtu mmoja (1) kati ya elfu mbili (2000) huzaliwa wakiwa na ulemavu wa ngozi wakati katika marekani ni mtu mmoja kati ya elfu kumi na saba ndio huishi na ulemavu wa ngozi. 
Mauaji ya Albino katika Tanzania yanaonekana kushamiri katika Mikoa ya kanda ya ziwa, ambapo imani za kishirikina zikitajwa kuwa chanzo kikubwa cha mauwaji ya hayo lakini pia yale yalio wahusu vikongwe yanayo husishwa na masuala ya kujipatia utajiri wa haraka suala ambalo sio la kweli, ambapo takwimu zinaonesha kuwa mauwaji yalianza siku nyingi japo kuripotiwa katika mamlaka za serikali na vyombo vya habari ilianza mwaka 2006/2007. 
Hivi sasa zipo asasi za kiraia zinazo jihusisha na harakati za kupinga mauwaji hayo ikiwapo asasi ya Under The Same Sun ya Nchini Canada na kwa Tanzania imeshakuwa na tawi toka mwaka 2008. 
KAMANDA WA POLISI. 
Awali akitoa taarifa ya uchunguzi wa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mulowola alisema tayari watu 15 wanashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani humo kwa mahojiano zaidi akiwapo baba mzazi wa Pendo, lakini pia jeshi hilo limefanikiwa kuipata piki piki iliyotumika kufanya unyama huo. 
“Hivi sasa tunawashikilia watu wapatao kumi na watano na wanaendelea kuhojiwa na Polisi” alisema Mlowola na kuongeza kuwa huo sio mwisho kwa kuwa jinai haina mwisho hata miaka ishirini tukio hili litaendelea kuchunguzwa”, na kusema hata kama yeye atahamishwa au kustaafu kijana atakayekuja ataendelea na kesi hiyo, hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kile wanacho kifahamu, alisema Mlowola na kusema tayari Jeshi hilo mkoani hapa limetangaza kutoa Milioni tatu 3 kwa atakayefanikisha kupatikana kwa mtoto Pendo. 
Mtoto Pendo alikuwa ni miongoni mwa alibino 74 waliopo katika wilaya ya Kwimba na alikuwa namba 9 katika suala la kupatiwa ulizi. 
Imeandaliwa na Afisa habari Mwanza- Atley Kuni.
BW.  ALFREDY KAPOLE MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WA MWANZA AKIZUNGUMZA KATIKA MKOA HUO.
 WAANDISHI WA HABARI SHEILA SEZI NA GRACE CHILONGOLA WALIPOKUWA WAKIONGEA NA MAMA YAKE NA PENDO.
 NYUMBANI KWAO NA MTOTO PENDO, MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WAMWANZA ALFREDY NA MWENYEKITI WA CHAWATA MKOA WAKIONGEA NA MAMA PENDO EMMENUEL.
 WANANCHI WA KIJIJI CHA NDAMI WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO HAYUPO HEWANI.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA AFANDE  VALENTINO MULOWOLA ALIPOKUWA AKITOA TAARIFA YA UCHUNGUZI HADI SASA
SUNGU SUNGU WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA.

JK RAIS KIKWETE ATEUA MWENYEKITI, MAKAMU MWENYEKITI NA MAKAMISHNA WANNE WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA



JK AKUTANA NA RAIS WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu Jaji Augustino  Ramadhani wakati jaji huyo alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es  Salaam leo. Picha na Freddy Maro


INTRODUCING SNOPPY ZONNER'S SINGLE "VUTA PUMZI (THE FACE.NOIZ)"


DKT. MAGUFULI AAGIZA KUFUNGWA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI KATIKA VIVUKO VYOTE NCHINI

Na JOHN DOTTO,  Mwanza 
 WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ameagiza kufungwa kwa mfumo mpya wa kielektroniki katika vivuko vyote nchini ili kukabiana na wajanja wachache wanahujumu mapato katika vivuko hivyo. 
 Mbali ya hilo, ameagiza kufanywa kwa utaratibu utakaowezesha huduma katika vivuko zinatolewa kwa saa 24 ili kukidhi mahitaji ya wananchi. 
 Dkt. Magufuli alitoa maagizo hayo jana katika uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania. 
 "Tulianze pale Kigamboni na tukaona mafanikio, tulipokuja hapa (Kigongo) tukaboresha na mafanikio yameonekana kwa kiasi kikubwa. Vivuko vyote sasa vifungwe mfumo mpya wa kielektroniki...vivuko vyote nchini," aliagiza Dkt. Magufuli. 
 Alisema mfumo huo una faida kubwa ikiwemo kudhibiti upotevu wa mapato ambapo katika kivuko cha kigongo - Busisi alisema mapato yameongezeka kwa takribani asilimia 40 baada ya kufungwa kwa mfumo huo. 
 Hata hivyo, Dkt. Magufuli alikataa kutaja ni kwa shilingi ngapi mapato hayo yameongezeka kwa hofu kuwa watu wenye dhmira mbaya wakisikia wanaweza kwenda na kufanya uhalifu. 
 Pia, aliagiza Kivuko kwa Kigamboni nacho kiboreshwe mfumo wake kama ilivyokuwa kwa Kigongo - Busisi. Waziri huyo wa Ujenzi, alisema kutokana na mafanikio yanayopatikana katika kudhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi, wafanyakazi husika kwa maana ya wale wa TEMESA maslahi yao yanapaswa kuangaliwa upya na kuboreshwa. "Kama mapato ni mazuri, wafanyakazi nao walipwe vizuri, wasikae kimasikini kwani wanapaswa kuona mwaka 2015 ni ukombozi katika maisha yao. 
 Alisema serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete imefanikiwa kujenga madaraja yote makubwa nchini ambapo kwa sasa kuna madaraja 4880 nchini na kuwa wakati inapata uhuru kulikuwa na madaraja mawili ambayo yalikuwa ya kuvutwa. 
 Mfumo wa kielektroniki katika vivuko vya Kigamboni na Kigongo Busisi ulifungwa na Kampuni ya Africom Tanzania ambaye Mkurugenzi Mtendaji wake Juma Rajabu alisema watahakikisha wanafunga mifumo ambayo itadhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi ambao ndiyo watumiaji.
Dkt. John Magufuli akikata utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Dkt. John Magufuli akikata utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Dkt. John Magufuli na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakifurahia baada ya kukata  utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Mfanyakazi wa  kivuko cha Kigongo -busisi mkoani Mwanza akionesha wananchi namna ya kutumia mashine hiyo

SERIKALI YAMPONGEZA PROFESA MBWETE KWA KUANZISHA MAKTABA BINAFSI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalum), Prof. Mark Mwandosya akizindua maktaba ya kisasa binafsi iliyoanzishwa na Prof. Tory Mbwete nyumbani kwake Mavurunza B. jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia uzinduzi huo ni Mama Halima Mbwete. Waziri Mwandosya amewataka wasomi hasa maprofesa kuiga mfano wa mwenzao ilikuweza kukuza elimu hapa nchini.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (kazi maalum),Prof. Mark Mwandosya akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria wa kwanza kilipo anzishwa, Prof. Geoffrey  Mmari walipokutana katika uzinduzi wa maktaba ya kisasa iliyo anzishwa na Makamu Mkuu chuo kikuu huria Prof Tory Mbwete (wa pili kushoto). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji TCU Bw.  Yunisi Mgaya. Maktaba hiyo ipo Mavurunza B nyumbani kwa Profesa Mbwete.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (kazi maalum),Prof. Mark Mwandosya akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na masoko wa Chuo kikuu huria Tanzania,Dr. Heriet Heller pamoja na wana kamati wenzake walio weza kufanikisha hafla hiyo ya uzinduzi.
Wageni waalikwa wakishuhudia uzinduzi.

MH. MAKALLA ZIARANI KWENYE JIMBO LA MVOMERO

Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akimkabidhi Kiongozi wa kikundi cha Faidika wa kijiji cha manza mchango wa shilingi laki tano.Mh. Makalla yupo Jimboni kwake Mvomero kwa ziara ya Kikazi.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwasalimia vijana wa kijiji cha manza,Mvomero wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi kwenye Jimbo la Mvomero.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akikabidhi mbuzi kumi kwa ajili ya walemavu kumi kijiji cha Chohero,Mvomero.

AG MASAJU: WATUMISHI WA UMMA TUFANYE KAZI KWA UZALENDO

Na Mwandishi Wetu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju amewakumbusha watumishi wa umma katika sekta ya sheria kufanya kazi kwa ushirikiano na uzalendo ili kulinda maslahi ya taifa.

Bw. Masaju, ambaye ameteuliwa na kuapishwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo, amefafanua kuwa watumishi wa umma wanapozingatia uzalendo katika utendaji wao, wanapata nguvu ya kusimama na kukemea maovu.

Bw. Masaju ameyasema hayo leo (Jumatano, Januari 7, 2015) jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria alipokwenda kubadilishana nao mawazo.    

“Sisi kama Wizara kwa ujumla wetu, tunapaswa kuwa mfano wa uzalendo katika taifa hili ili tunaposimama mbele ya watu, tuwe na nguvu kwa kuwa tupo safi,” amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye kabla ya uteuzi huo, alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro alimpongeza Bw. Masaju kwa heshima aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete na kuahidi kuwa yeye na Wizara itaendelea kumpa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake.

“Tunakupongeza kwa heshima kubwa uliyopewa na Mheshimiwa Rais na sisi kama wasimamizi wa sera, tutaendelea kutoa ushirikiano kwako kama tulivyofanya kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyetangulia,” alisema Waziri Migiro.

Aidha, Waziri Migiro aliahidi kuongeza ushirikiano katika kuimarisha kada ya Mawakili wa Serikali pamoja na watumishi wengine ili kuongeza ufanisi katika utoaji haki.

Bw. Masaju aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali tarehe 2 Januari mwaka huu na kuapishwa tarehe 5 Januari. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Aidha, Bw. Masaju amewahi kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju (kushoto) akikaribishwa Wizara ya Katiba na Sheria kwa shada la maua kutoka kwa mtumishi wa Wizara Bi. Christina Jenga leo (Jumatano, Januari 7, 2015) jijini Dar es Salaam huku Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Maimuna Tarishi akishuhudia. Bw. Masaju alifika Wizarani kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais Jakaya Kikwete ili kubadilishana mawazo na viongozi na watumishi wa Wizara.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju akipokewa na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria leo (Jumatano, Januari 7, 2015) wakati alipofika Wizarani hapo kukutana na viongozi na watumishi ili kubadilishana mawazo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro leo (Jumatano, Januari 7, 2015) wakati alipofika Wizarani kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais jakaya Kikwete hivi karibuni.

BALOZI WA COMORO NCHINI AKUTANA NA RAIS DK.SHEIN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Comoro Nchini Tanzania Dk.Ahamada El Badaoui Mohamed alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa mazungumzo na Rais .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Comoro Nchini Tanzania Dk.Ahamada El Badaoui Mohamed alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo .Picha na Ikulu.

ZIARA YA WAZIRI MKUU PINDA KATIKA JIMBO LAKE LA UCHAGUZI

 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea  silaha za jadi, upinde, mishale na usinga kutoka kwa  Machifu wa kabila la Wakonongo  katika mji wa Inyonga wilayani Mlele akiwa katika ziara ya jibo lake la uchaguzi Januari 7, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mlele baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Halmashauri hiyo kuhutubia mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Januari 7, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanawake wa  Nsimbo wakati alipowasili kwenye viwanja vya Halmashauri hiyo kuhutubia mkutano wa hadhar akiwa katika ziara ya jimbi lake la uchaguzi Januari7, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni