Jumatatu, 8 Desemba 2014

MASHINDANO YA BIBLIA YAFANYIKA UWANJA WA KAITABA BUKOBA

Msanii wa muziki wa Injili, Bonny Mwaitege(kulia) akisalimiana Mtangazaji wa Radio Kasibante Mwl. Joyce Ruboz punde leo hii wakati wa kipindi cha Gospal flava cha Kasibante fm 88.5, Rose Muhando, Bonny Mwaitege na Gaston Sapula wanatarajia kupamba fainali za Mashindano ya Biblia leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba mjini kuanzia saa 8 Mchana. Shindano hili lililokuwa likiendelea hapa Bukoba na kuzikutanisha Wilaya mbalimbali zikiwemo Wilaya ya Muleba, Karagwe, Misenyi na sasa kufikia tamati leo hii Jumapili Dec. 5. Fainali ambazo zitafanyika leo na Mgeni Rasmi ni Mbunge wa Bukoba Mjini(CCM) Mh. Khamis Sued Kagasheki. Mtumishi wa Mungu na muimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando akiwa kwenye Ofisi za radio Kasibante Fm 88.5 akionekana mwingi wa Furaha huku akiteta jambo na Mtangazaji katika live ya kipindi cha Gospal Flava leo ambapo wamepata fursa ya kuongea na Wananchi na kuwataka kusogea baadae katika Fainali za Biblia zitakazofanyika leo kwenye Uwanja wa kaitaba Bukoba Mjini. Mtangazaji wa kipindi cha Gospal Flava Mwl. Joyce Ruboz akifurahia jambo baada ya kuwaona Waimbaji wa Injili wakiporomosha sauti zao tamu wakati wa kipindi chake leo Asubuhi. Mwalimu Joyce Ruboz pia ni Mmoja wa Waratibu wa Fainali hizi za Biblia hapa Bukoba katika swala zima la Kutanua na kuendeleza jamii kupitia Vipindi vya Dini. Wasanii hao Kutoka Jijini Dar es salaam Rose Muhando, Bonny Mwaitege na Gaston Sapula walitinga ndani ya Radio Kasibante fm na tayari kupamba fainali za mashindano ya Biblia leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba kuanzia saa 8 MchanaBoniface Mwaitege akiwa na Msanii mwenzake wa Nyimbo za Njili Gaston Sapula kwenye Studio za radio kasibante Fm Bukoba. Rose Muhando akiwa na Gastona SapulaRose Muhando akiwa Katika Ukumbi wa Radio Kasibante FmMtangazaji wa radio kasibante Fm 88.5 Abera nae alikuwepo na hapa akionekana wa furaha baada ya kukutana tena na Rose Muhando katika Ofisi zao za radio kasibante Fm.

Picha ya pamoja Mwalimu Joyce Ruboz na Wasanii wa Injili wanaotarajia kupamba fainali za Biblia leo katika Uwanja wa Kaitaba.Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera (RPC) Henry Mwaibambe nae alipata picha ya pamoja na wasanii hao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni