Maombolezo ya majonzi yametolewa katika mazishi ya nahodha wa timu ya mpira ya Afrika Kusini, Senzo Meyiwa.
Mauaji yake Jumapili iliyopita yalishtusha nchi nzima.
Wajumbe wa serikali, wachezaji mpira pamoja na watu maarufu walijumuika na maelfu ya washabiki katika uwanja mkuu wa mpira mjini Durban, kwa mazishi ya kijana ambaye akitarajiwa kuzidi kunawiri kwenye mpira siku zijazo.
Watu wengi walivaa t-shati za picha ya Meyiwa.
Senzo Meyiwa alipigwa risasi na kuuwawa Jumapili akiwa na umri wa miaka 27 alipopambana na wezi wawili katika nyumba ya mchumba wake karibu na Johannesburg.
Mauaji yake yamezusha hasira na kufufua mjadala kuhusu vipi Afrika Kusini inaweza kupunguza wizi wa kutumia nguvu.
Mtu mmoja ameshtakiwa kwa mauaji hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni