Wahitimu akiwa katika picha ya pamoja
DC Madaha pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu
Mkuu wa wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Bw.Juma Solomon Madaha amewataka wananchi wilayani hapa kutobeza shule za jumuhiya ya wazazi ccm Tanzania kwani tokea awali ndizo zilizokuwa zikitoa elimu ya Sekondari bila kujari itikadi za vyama vingine vya siasa nchini.
Bw.Madaha aliyasema hayo katika hotuba yake hivi karibuni kwenye mahafari ya kidato cha nne akiwa mgeni rasmi katika shule ya Sekondari Ludewa mjini ambayo inamilikiwa na umoja wa wazizi wa chama cha mapinduzi ambapo shule hiyo awali ilikuwa na wanafunzi zaidi ya 800 lakini hivi sasa inawanafunzi chini ya 400.
Alisema shule hiyo imekuwa mkombozi katika wilaya ya Ludewa kwa kutoa elimu bora na ufauru wa hali ya juu lakini kuna baadhi ya watu wanashindwa kupeleka watoto wao eti kwa kua shule hiyo ni ya Chama Cha Mapinduzi dhana ambayo si sahihi kwani hakuna chama cha siasa ambacho kimeanza kusoma kidato cha kwanza na kuhitimu kidato cha nne.
Bw.Madaha alisema hakuna shule ya Sekondari nchini ambayo inafundisha masomo ya chama cha siasa hicho hayo ni mawazo mgando na yanapaswa kupigwa vita ili yasitengeneze kasumba mbaya kwa watoto wanaohitaji elimu ili iwasaidie katika maisha yao.
“shule za umoja wa wazazi wa ccm nchini hazifundishi masomo ya chama bali ni sirabasi za wizara ya elimu hivyo wazazi mnapaswa kuzitumia shule hizi ambayo ni mkombozi kwa maisha ya watoto wenu na hakuna chama ambacho kipo darasani zaidi ya watu wakipata elimu ndio wanakwenda kuanzisha vyama vya siasa,hivyo tuache fikla potofu zaidi ya kuawaendeleza watoto wetu”,alisema Bw.Madaha.
Aidha mwenyekiti wa bodi ya shule ya Ludewa Sekondari na Diwani wa kata ya Ludewa mjini Mh.Monica Mchilo aliwataka baadhi ya wanaume wenye tabia ya kuwarubuni wanafunzi wa kike na kuwakatisha masomo kuacha mara moja tabia hiyo kwani ni kinyume na maadiri ya kiafrika.
Alisema kumekuwa na baadhi ya akina baba na vijana huwarubuni wanafunzi hao na baadae kuwapa ujauzito na kuwatelekeza katika hali mbaya ya kimaisha bila ya kufikiria kuwa nao wanamabinti kama hao ambao wako katika shule nyingine wakipata elimu kama walivyo wa Ludewa Sekondari.
Mh.Monica alisema kama kuna manaume anazipenda sana sketi za shule basi anaweza kumnunulia mke wake azivae ili aongeze upendo kuliko kuwafuata watoto wa shule na kuwaharibia ndoto zao za maisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni