Taarifa kutoka nchini Zambia zinasema
kuwa Rais wa nchi hiyo,Michael Sata amesafiri nje ya nchi kwa matibabu kufuatia
taarifa kuwa afya sio nzuri.
Taarifa kutoka kwa ofisi ya Bwana
Sata mwenye umri wa miaka 77 ilisema Rais amekwenda nje kwa matibabu ingawa
haikusema ni katika nchi gani.
Rais Sata alijitokeza hadharani
tarehe 19 Septemba kuambia bunge la taifa kuwa bado yuko hai.''Mimi sijafa''
alinukuliwa akisema Sata.
"Anajulikana kama ''King
Cobra" kwa kauli zake kali, na alichaguliwa Raia wa Zambia mwaka 2011.
Haijabainika ikiwa atarejea Ijumaa
kuongoza sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo.
Bwana Sata hajaonekana hadharani
tangu kurejea kutoka katika mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa mwezi jana
ambako alikosa kutoa hutuba aliyotarajiwa kutoa.
Waziri wa ulinzi , Edgar Lungu,
ameteuliwa kama Rais wa muda kufuatia hali mbaya ya afya inayokabili Rais
Michael Sata.
CREDIT: BBC/SWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni