Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetumia jumla ya
shilingi milioni 731,360,000/= kusaidia miradi ya vijana ya kufyatua tofali
nchini.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma na
Mawasiliano wa NHC, Bi Suzan Omari wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Vijana
kilichofanyika hivi karibuni mkoani Tabora.
Bibi Suzan amefafanua kuwa fedha hizo zinahusisha
ununuzi wa mashine uliyogharimu shilingi 297,000,000/=, mafunzo ya wakufunzi
yaliyogharimu shilingi 47,000,000/= na uwezeshaji mtaji wa kuanzia kazi
za vikundi vya vijana kufyatua matofali shilingi 81,500,000/=.
Ameongeza kuwa matumizi mengine kuwa ni usambazaji wa
mashine uliyogharimu shilingi 30,000,000/=, uhakiki wa ubora wa mashine
uliofanywa na wataalamu kutoka VETA shilingi 6,400,000/=, fedha za kununulia
vifaa vya mafunzo katika kila halmashauri vilivyogharimu shilingi 130,400,000
na posho ya wakufunzi wa VETA ni shilingi 139,060,000/=.
Bi Suzan amewataka vijana kote nchini kutumia fursa hii
kwa ajli ya maendeleo yao ikiwemo na kuondokana na tatizo la kukukosa ajira.
Amayetaka mashirka mengine nchini kuiga mfano wa NHC ili kunusuru nguvu kazi
hii kubwa.
Kwa upande mwingine, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC,
Bw, Muungano Saguya amesema kuwa wadau zikiwemo Halmashauri, Maafisa Vijana wa
Mikoa na wilaya kwa kushirkiiana na mamameneja wa mikoa wa NHC wathamini mradi
huu kwa kufuatilia ufanisi wake ili mradi huo uwe endelevu.
Ameongeza kuwa mradiukiwa endelevuna kusaidia kupunguza
tatizo la ajira kwa vijana, bajeti itaongezeka kwa mwaka wa fedhaujao
ilikusaidia zaidi mradi huo kwa vijana.
Naye Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa
Tabora, Bw. Erasto Chilambo amesema maafisa vijana wawaunganishe vijana katik a
vikundi ili watumie fursa hii kujiendeleza na kuacha kubweteka na kulalamika
kwa kukosa ajira.
Aliongeza kuwa vijana wasiwe sehemu ya tatizo la
ajira bali wawe watatuzi wa changamoto inayowakabili ya kukosa ajira.
Kikao hiki ni kikao cha kuwakumbusha maafisa vijana
majukumu yao kuwasaidia kupata uzoefu toka kwa wenzao. Kimeandaliwa na
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni