Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetumia jumla ya shilingi
milioni 731,360,000/= kusaidia miradi ya vijana ya kufyatua tofali nchini.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Mawasiliano wa
NHC, Bi Suzan Omari wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Vijana kilichofanyika hivi
karibuni mkoani Tabora.
Bibi Suzan amefafanua kuwa fedha hizo zinahusisha ununuzi
wa mashine uliyogharimu shilingi 297,000,000/=, mafunzo ya wakufunzi
yaliyogharimu shilingi 47,000,000/= na uwezeshaji mtaji wa kuanzia kazi
za vikundi vya vijana kufyatua matofali shilingi 81,500,000/=.
Ameongeza kuwa matumizi mengine kuwa ni usambazaji wa mashine
uliyogharimu shilingi 30,000,000/=, uhakiki wa ubora wa mashine uliofanywa na
wataalamu kutoka VETA shilingi 6,400,000/=, fedha za kununulia vifaa vya
mafunzo katika kila halmashauri vilivyogharimu shilingi 130,400,000 na posho ya
wakufunzi wa VETA ni shilingi 139,060,000/=.
Bi Suzan amewataka vijana kote nchini kutumia fursa hii kwa ajli
ya maendeleo yao ikiwemo na kuondokana na tatizo la kukukosa ajira. Amayetaka
mashirka mengine nchini kuiga mfano wa NHC ili kunusuru nguvu kazi hii kubwa.
Kwa upande mwingine, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Bw,
Muungano Saguya amesema kuwa wadau zikiwemo Halmashauri, Maafisa Vijana wa
Mikoa na wilaya kwa kushirkiiana na mamameneja wa mikoa wa NHC wathamini mradi
huu kwa kufuatilia ufanisi wake ili mradi huo uwe endelevu.
Ameongeza kuwa mradiukiwa endelevuna kusaidia kupunguza tatizo
la ajira kwa vijana, bajeti itaongezeka kwa mwaka wa fedhaujao ilikusaidia
zaidi mradi huo kwa vijana.
Naye Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Tabora,
Bw. Erasto Chilambo amesema maafisa vijana wawaunganishe vijana katik a vikundi
ili watumie fursa hii kujiendeleza na kuacha kubweteka na kulalamika kwa kukosa
ajira.
Aliongeza kuwa vijana wasiwe sehemu ya tatizo la ajira
bali wawe watatuzi wa changamoto inayowakabili ya kukosa ajira.
Kikao hiki ni kikao cha kuwakumbusha maafisa vijana majukumu
yao kuwasaidia kupata uzoefu toka kwa wenzao. Kimeandaliwa na Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni