Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred ijulikanayo kwa jina na Brigitte Alfred Foundation (BAF) ikishirikiana na taasisi ya Junior Achievement Tanzania (JAT) inazindua rasmi mafunzo ya ujasiriamali kwa jamii ya Albino.
Akizungumza katika
uzinduzi huo jana, Brigitte alisema kuwa taasisi yake kwa kushirikiana na JAT
itaanza na mafunzo kwa albino 50.
Brigitte alisema kuwa
mafunzo hayo yanalenga sehemu kuu mbalimbali ambazo ni kujitambua (Life skills),
kutathmini aina mbalimbali za biashara (Business Analysis), namna ya kutunza
pesa ( How to save), kuandika mchanganuo wa biashara (Business Plan),
kutembelea sehemu mbalimbali zinazoendana na biashara atakayoifanya na jinsi ya
kuanza biashara.
Alisema kuwa BAF
ikishirikiana na wadau mbalimbali na pia itagharimia gharama za mafunzo na
mahitaji mbalimbali ya kuboresha hali yao.
“Mafunzo haya yatachukua
muda wa mwaka mmoja yaani watashiriki na yataanza rasmi Agosti 18, kila
mshiriki wa mafunzo haya atapatiwa kitabu chenye masomo yote ili aweze
kuendelea kujisomea,” alisema Brigitte.
Mkurugenzi wa JAT, Maria
Ngowi alisema kuwa wamejipanga kufanikisha mpango huo na wanaamini albino
watakaopata mafunzo hayo watafanikiwa katika maisha yao ya kila siku. Ngowi
alisema kuwa JAT imejikita katika Nyanja tatu ambazo ni ujasiria mali, elimu ya
kuzalisha, kuiwekeza na kutunza fedha na elimu ya kazi.
Alisema kuwa taasisi yao
ni sehemu ya taasisi kubwa ulimwenguni inayoitwa Junior Achievement
International ambayo iko katika nchi 120 duniani huku afrika ikiwa katika nchi
17.
Kaimu Katibu Mkuu wa
Tanzania Albino Society (TAS), Mohamed Chanzi alimshukuru Brigitte na JAT kwa
kuwajali na kuomba wadau mbali mbali kuwaunga mkono.
“Wamelenga kutusaidia
kimaisha, kwani msaada wa elimu ni mkubwa kulinganisha misaada mingine, naomba
wadau wawaunge mkono,” alisema Chanzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni