Alhamisi, 15 Desemba 2016

Mwanzilishi wa tovuti ya JamiiForums,akamatwa na Polisi


Mwanzilishi wa tovuti ya JamiiForums, Maxence Melo amekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam kwa kukataa kutoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo.

Taarifa kutoka kwenye tovuti hiyo zinaeleza kuwa Melo amenyimwa dhamana hivyo atalazimika kukaa rumande mpaka kesho atakapofikishwa mahakamani.

Jeshi la Polisi linadai kuwa Melo amekataa kuonyesha ushirikiano kwa Jeshi hilo ambapo walikuwa wakihitaji majina ya baadhi ya watumiaji wa mtandao huo.

JamiiForums wameeleza kuwa kiongozi huyo (Maxence) alikataa kutoa taarifa hizo kwa kile alichoeleza kuwa kufanya hivyo ni uvunjwaji wa Sheria na Haki za wananchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni