Jumamosi, 6 Juni 2015

Urais 2015: Mwigulu achukua fomu,

Asema Kikwete ni Rais wa Mwisho 

Kutawala Tanzania Masikini

Mpekuzi blog
Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba pamoja na Mke wake katika ukumbi wa makao makuu ya CCM Dodoma.
 

Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akiongea na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa NEC Dodoma.
Mke wa Mwigulu Nchemba akiwasalimia Waandishi wa Habari.
Naibu waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba katika mkutano na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais leo.

Naibu Waziri waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba leo amechukua  fomu ya kugombea urais wa  Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa atateuliwa  na chama chake cha Mapinduzi kupeperusha bendera  ya Tanzania katika uchagauzi mkuu ujao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari amesema kwamba atahakikisha anaboresha uchumi kwa  wananchi, ikiwa ni  pamoja na kuboresha njia kuu za wananchi kupata kipato. Kufufua viwanda vilivyokufa  ili kutoa ajira kwa vijana pamoja na  kudhibiti madawa ya Kulevya, Rushwa na ufisadi.

Amesisitiza kuwa Rais Kikwete ndiye rais wa mwisho kutawala Tanzania maskini.
Mpekuzi blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni