Alhamisi, 4 Juni 2015

'Mimba' Ya Lulu Michael Yapotea

Mpekuzi blog

Miezi miwili iliyopita kuliibuka madai mazito kwamba staa bei mbaya wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameongezeka tumbo hivyo mashabiki wake wakapiga vigelegele kwamba huenda ana mimba lakini sasa tumbo hilo limeyeyuka.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Lulu kwa sasa anakatiza viunga vya chuo anachosoma cha Magogoni jijini Dar akichukua masomo ya Uhusiano wa Umma, akiwa hana lile tumbo la Aprili.
Mwandishi alizungumza na baadhi ya wanafunzi wenzake ambao walidai msanii huyo alikuwa hafiki chuoni hapo kwa muda mrefu lakini sasa amejaa tele ‘mwepesii’.
  
“Hakuwa akija chuoni kwa muda, baadaye akawa anahudhuria kwa ‘kupibu’ kisha kuacha tena ila ameanza juzi tu kutokana na kuwepo kwa mitihani,” alisema mmoja wa wanachuo hao.
Kama taaluma inavyoelekeza, mwandishi wetu alimtafuta Lulu kupitia simu yake ya mkononi huku ikiita bila majibu.
Baadaye alitumiwa ujumbe wa  kuulizwa  kuhusu  sakata  hilo  ambapo   alijibu: “Hao wanaodai nina mimba walinipa wao? Sina nafasi ya kufafanua.” 
Hivi karibuni Lulu aliripotiwa na mitandao ya kijamii kuwa huenda ana mimba.

Chanzo: Gpl/Gazeti  la  Amani
Mpekuzi blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni