MH. SITTA APEWA CHEO CHA MWIZUKULU MKULU WA UNYANYEMBE!
Mtemi wa Unyanyembe Msagata Ngulati Fundikira akimtambikia Mh Samuel Sitta ambaye ni binamu yake. Mtemi wa Unyanyembe Msagata Ngulati Fundikira leo hii asubuhi alimpa cheo chaMwizukulu mkulu Mh Samuel Sitta katika kutambua safari yake ya kukiomba chama chake cha CCM kimpe ridhaa ya kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao. |
Mh Samuel Sitta akiwa na mkewe Mh Magreth Sitta wakisubiri kutambikiwa. |
Mtemi wa Unyanyembe Msgata Fundikira akisisitiza jambo katika hafla fupi ya kumpa cheo Mh Samuel Sitta |
Mtemi Msagata akimvika mgololoMh Sitta |
Mtemi Msagata Fundikira, Mh Rageh, Mh Samuel Sitta na Mlinzi Mh Sitta wakitokea sehemu maalumu palipofanyika tambiko. |
Picha na Habari na Mkala Fundikira wa TBN CENTRAL ZONE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni