MH. SAMIA SULUHU AENDELEA NA ZIARA YA KUKAGUA SHUGHULI ZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA WILAYANI MUHEZA, TANGA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kijiji cha UWAMAKIZI alikoenda kwenye ziara ya kukagua shughuli za utunzaji wa mazingira katika kijiji cha Bombani kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akiongea na baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Bombani wilayani Muheza mkoani Tanga alipotembelea kijijini hapo katika maadhimisho ya wiki ya siku ya Mazingira duniani insyofanyika jijini Tanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akifurahia mbegu ya milimao inayooteshwa na wanakikundi wa kikundi cha UWAMAMKIZI katika kijiji cha Shembakazi wilayani Muheza mkoani Tanga.
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Anjelina Madete akiongea na wanachama wa Kikundi cha nguvu kazi wanaohusika na uoteshaji wa mbegu za miti na matunda pamoja na kutunza mazingira katika kijiji cha Mashewa wilayani Muheza mkoani Tanga.
@http://issamichuzi.blogspot.com/
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni