Jumapili, 14 Juni 2015

BREAKING NEWS AJALI MBAYA YADAIWA 
KUUA ABIRIA 22 IRINGA



WATU  22  wamepoteza maisha  usiku   huu katika ajali ya  gari aina  ya costa mali ya Another G inayofanya  safari  zake kati ya Njombe - Iringa baada ya  kugongana na  Lori.

Taarifa za  awali  ambazo  mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz  umezipata  kutoka  eneo la tukio zinadai kuwa ajali hiyo imetokea  eneo la Kinyanambo nje  kidogo na mji wa Mafinga wilaya ya  Mufindi  mkoani Iringa wakati  gari hiyo ya Another G ikitokea  Njombe  kwenda Iringa

Mbali ya  kuwa maiti ambazo  zimetolewa na  kufikishwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya wilaya ya  Mufindi kuwa  zimekwisha  fika zaidi ya 10 ila inadai kuwa idadi ya  miili  inaweza kuongezeka  zaidi kutokana na kazi ya  uokoaji  ikiendelea eneo la tukio.

Imeelezwa  kuwa  waliopoteza  maisha ni wanaume 15 na wanawake 7 huku majeruhi 34 ambao wamelazwa katika Hospitali ya  wilaya ya  Mufindi 

Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi Mboni Mhita ameuthibitishia mtandao  huu wa matukiodaima kwa njia ya  simu juu ya ajali   hiyo na  kueleza kuwa ni  miongoni mwa ajali  mbaya kutokea  wilayani Mufindi .



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni