Huyu shabiki amewezaje kuingia mpaka chumbani kwa Chris Brown?? Akachora mpaka ukuta na magari ya jamaa..
Ni siku chache zimepita toka Chris Brown aingie kwenye headlines za kuhusishwa na ugomvi Las Vegas.. labda hiyo sio kitu kigeni kukisikia eti Chris kuhusishwa kwenye matukio ya aina hiyo !!.. Baadae ikaonekana hakuhusika.
Leo Chris Brown karudi tena.. hii ishu imechukua uzito wa juu sana mitandaoni, yani shabiki wa Chris Brown kashtakiwa na Chris… alivunja vitasa vyote vya milango ya kwenye nyumba ya Chris, akatupa nguo za mtoto wa Chris Brown nje pamoja na vitu vya mbwa wake.
Hakuishia hapo, aliandaa chakula kwa ajili yake na Chris Brown.. alafu akaandika “I love you” kwenye ukuta wa nyumba ya Chris Brown.
Akachora pia na magari ya Chris >>“I Love You”
Hii ilimshtua sana Chris, akaweka picha Instagram na post aliyoandika kwamba anapenda mashabiki wake ila ushabiki wa huyu ulimshtua.. kesi iko Mahakamani tayari na msichana huyo Amira Kodcia Ayeb huenda akahukumiwa mpaka miaka 7 jela.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni