Msemaji wa rais wa Burundi amesema kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza hatahudhuria mkutano wa kimaeneo ambao utaangazia mzozo ulio nchini mwake.
Msemaji huyo aliliambia shirika moja la habari la Ufaransa kuwa pierre Nkurunziza atakuwa akifanya kampeni ya uchaguzi wa urais na kwamba waziri wa mashauri ya kigeni ndiye atahudhuria mkutano ambao utawajumuisha marais wa Rwanda, Uganda , Tanzania na Kenya mjini Dar es Salaam.
Wakati Nkurunziza alihudhuria mkutano kama huo mpema mwezi huu baadhi ya maafisa wa kijeshi walijaribu kumpindua. Burundi imekumbwa na ghasia tangu Nkurunziza atangaze kuwa atawania urais kwa muhula wa tatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni