MH. EDWARD LOWASSA AANZA "SAFARI YA MATUMAINI" JIJINI ARUSHA
Gari iliyombeba Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama
cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward
Lowassa ikipita nje ya uwanja wa Sheih Amri Abeid, jijini Arusha mapema leo
asubuhi wakati akielekea kwenye Ofisi za CCM Mkoa. Mh. Lowassa anatarajia
kulihutubia taifa mchana wa leo kwenye uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,
ikiwa ni sehmu ya kutangaza kwake nia yake ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa
akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuwepo kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa
Arusha.Kulia ni Mkewe Mama Regina Lowassa.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisaini
kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha. Kushoto ni
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole
akizungumza machache mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama
cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward
Lowassa alieambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa pamoja na wanaCCM wengine.
Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina wakimsikiliza Mwenyekiti
wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole (hayupo pichani).
PICHA ZAIDI ZITAWAJIA BAADAE KIDOGO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni