Ijumaa, 29 Mei 2015

Kim anukia Simba, Hall atua Azam


Kim Poulsen 
Habari za uhakika kutoka klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi zilieleza kuwa Poulsen anayefundisha Silkeborg IF ya Ligi Kuu ya Denmark anatarajiwa kutua nchini wakati wowote kwa lengo la kusaini mkataba wa kuinoa timu hiyo.
Poulsen anasemekana kuwa atasaidiwa na kocha wa makipa aliyekuwa kocha akiifundisha Kenya Harambee Stars ya Kenya, Adel Amrouche.
Amrouche, raia wa Ubelgiji aliwasili nchini wiki iliyopita na kufanya mazungumzo na Simba na sasa habari zinaeleza kuwa atafanya kazi na Poulsen, anayetajwa kuchukua mikoba ya Mserbia Goran Kopunovic.
Goran aliyeinoa timu hiyo kwa muda mfupi msimu uliomalizika alitaka kulipwa dau kubwa ili aendelee kuinoa timu hiyo.
Kauli zenye utata
Mmoja wa viongozi wa klabu hiyo aliliambia gazeti hili kuwa Poulsen amekubali kimsingi kujiunga na klabu hiyo kwa dau la Sh30 milioni kama fedha za usajili na atakuwa akipokea mshahara wa Dola 8,000 kwa mwezi.
“Kulikuwa na makocha sita waliowania nafasi ya Goran, wakachujwa na kubaki watatu, wakiwamo Bob Williamson, Amrouch, lakini uongozi wa Simba ulikaa ukapitia maombi yao na kumjadili kwa kila mmoja na wameridhia kuwa na Poulsen ndiye anayefaa.
“Kikubwa kilichovutia ni Poulsen ambaye ni mvumilivu, amekuwa akitamani mafanikio na rekodi yake kwa Taifa Stars ndiyo yaliyombeba,” alieleza mmoja wa viongozi wa klabu hiyo.
“Viongozi wamejadili kila kitu na Kim ndiye wamekubaliana naye, suala la mshahara na kila kitu kipo wazi. Yeye (Poulsen) amewaeleza mshahara, mwisho wamekubaliana,” alieleza mtoa habari huyo.
Asemavyo Hanspoppe
Alipoulizwa kuhusu kocha mpya, mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hanspoppe aliliambia gazeti hili kuwa mchakato wa kumpata kocha mpya uko kwenye hatua za mwisho
.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni