Jumatano, 27 Mei 2015

JIVUNIE UTANZANIA NA DOT TZ (.TZ)


Kama utakuwa na kumbukubu nzuri kipindi cha nyuma kidogo ulikuwa ukiingia kwenye mtandao utakuta domain nyingi ziko kwa namna ya jinafulani.com alafu baada ya muda tukaanza kuona jinafulani.co.uk ila hapakuwa na jinafulani.co.tz. Hilo lime badilika na kwa 

Tanzania Network Information Centre (tzNIC) ni msajili wa domain zinazo ishia na .tz. Hivyo pale unapo taka kusajili domain ambayo inaishia na .tz hawa ndio wahusika wakuu. tzNIC wanasimamia mfumo ambao una onyesha barua pepe yani email na servers zote zinazo ishia na .tz na zilipo. Tanzania Network Information Centre nishirika lisilo la kutafuta faida (nonprofit) ambalo lilianzishwa na kusajiliwa mwaka 2006 kwaajili ya kusimamia na kutekeleza shuguli zote zinazo husiana na Tanzania country code Top Level Domain (.tz ccTLD). 

tzNIC ni limited company (kwa dhamana) ambayo ina waanzilishi wawili ambao ni TCRA ambae ni mdhibiti mkuu wa maswala ya mitandao Tanzania na TISPA (Tanzania Internet Service Provider Association) ambae ni sehemu ya chama cha ISP (Internet Service Provers Association).

Lengo la tzNIC

Lengo kuu la tzNIC ni kukuza matumizi ya majina ya domain yanayo ishia na .tz pamoja na kulinda maslahi ya walio sajiliwa kwa kuwapa database ambayo ina ulinzi wa kutosha na unafuu. Kwa kufanya hivyo huwapa watumiaji fursa ya kuonekana dunia nzima, wana brand huduma yako na muonekano wa kitanzania, kuongeza ushindani wa biashara yako ndani na nje ya Tanzania, kuwezesha domain yako ulio sajili kupata watembeleaji wengi wa ndani ya nchi ya Tanzania, na kukuza utumiaji wa mtandao katika biashara.

Wako wapi
Head office za tzNIC (Tanzania Network Information Cetre) ziko Suite #4 Ground Floor, of LAPF Millenium Towers, at the New Bagamoyo Road, Dar es Salaam na namba zao za simu ni +255 22 2772659 fax: +255 22 2772660 na email address ni:info@tznic.or.tz hivyo pale unapo taka ku register domain yako au una tatizo linalo husiana na usajili wa domain usisite kuwasiliana nao au kuwatembelea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni