Ijumaa, 29 Mei 2015

ISHU YA MISS TANZANIA YAINGIA TENA BUNGENI, WABUNGE HAWAITAKI KISA MAVAZA YANAZALILISHA WANAWAKE


Kwenye maswali na majibu ndani ya Kikao cha Bunge kibachoendelea Dodoma kuna vingi vinatokea, sasa hivi ni mijadala ya Bunge la Bajeti lakini ikifika wakati wa maswali na majibu kuna ishu nyingine huwa zinaibuliwa humohumo.. Leo niliinasa hii ya mashindano ya Miss Tanzania, kumbe kuna Wabunge hata hawayataki mashindano hayo kabisa !!

“Mimi sioni haja ya mashindano ya mamiss Tanzania.. Sisi tunaongozwa na maadili, unamuona mtoto wako anaenda kushindana mamiss, na ipo Kitaifa kabisa MheshimiwaFenela? Unamuona mtoto anavyodhalilishwa kwa sababu ya gari.. Jamani kama hamna gari bora mpande baiskeli au mpande pikipiki majumbani mwenu“>>>Mbunge Faida Mohamed Bakari.

“Sisi wazazi hasa wanawake hatutaki.. Serikali inashadadia umiss hasa mimi nasema huu umiss una faida gani katika nchi yetu? Mbona hawafanyi na wanaume?“>>> Faida Mohamed Bakari.


“Pamoja na yale mapungufu ambayo ameyagusia miss Tanzania ni suala la kisanii na yale mapungufu yalifanyiwa kazi na tukaruhusu Miss Tanzania ikaendelea“>>> Fenela Mukangala.

Ikafika time ya maswali kujibiwa >>> “Miss Tanzania inatengeneza ajira kwa warembo na pia inatangaza nchi na vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi na pia inatoa burudani na elimu. Tunao warembo wenye akili nzuri wanaotumia nafasi ya Miss Tanzania kutengeneza ajira kwa vijana wengine“>>> Waziri Fenela Mukangala.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni