Ili Aweze Kuzaa, Wema Sepetu ni Lazima Alale Juu ya Kaburi au Arithiwe na Ndugu Yake Steven Kanumba
Mpekuzi blog
Baba mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, Charles Kusekwa Kanumba amefunguka kuwa ili azae, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anatakiwa alale juu ya kaburi.
Hayo yanakuja siku chache baada ya Wema aliyewahi kuwa mchumba wa Kanumba kudai kusumbuliwa na tatizo la kukosa uwezo wa kuzaa hivyo mzee huyo kujiongeza na kusema ni kwa sababu alitoa mimba ya mwanaye huyo.
Akizungumza na waandishi wetu, baba huyo alisema kama kweli Wema alitoa mimba ya Kanumba basi atakuwa alijilaani kwa sababu ukoo wao ukitoa mimba unaweza kufa au kujilaani (kutokupata mtoto) hivyo anatakiwa kutambika kwa kulala juu ya kaburi la mama mkubwa wa Kanumba ambaye ni bibi wa babu wa mzee Kanumba.
Alisema sambamba na hilo, Wema atatakiwa kurithiwa na ndugu wa Kanumba (kati ya kaka au mdogo wake).
“Kwenye ukoo wetu ukitoa mimba kuna mambo mawili, moja ni kufariki dunia au ‘kujikila’ (kujilaani) kwa kutokuzaa, pengine ndicho kilichomtokea Wema,’’ alisema baba Kanumba.
Mzee huyo alisema kuwa mama mkubwa huyo alishafariki dunia kwa hiyo yeye na marehemu Kanumba walipaswa kwenda kaburini kwake kufanya tambiko zito, wakiwa wamevaa mavazi maalumu ya kiasili na mikononi wameshika vibuyu, jambo ambalo lingempasa Wema kukaza moyo.
Alisema kuwa wakiwa kaburini hapo, Wema alitakiwa achotewe mchanga na kushikishwa kisha kusemewa maneno ya kuomba msamaha kwa kilichotokea.
Alisema walitakiwa waende na maziwa, unga wa mtama na hayo mavazi maalumu kwa ajili ya tambiko hilo.
Aliendelea kudadavua kwamba, kwa sasa Kanumba hayupo duniani hivyo Wema anapaswa kuchukuliwa na kaka au mdogo wake wa damu kwenda kutambika, ikiwa ni pamoja na kuzaa naye ili kufungua mlango wa kizazi, hata kama ataachika basi ataendelea kupata watoto.
Baba Kanumba alisema mama mkubwa huyo ni bibi yake mzee Charles Kanumba ambaye katika ukoo wao alikuwa mganga wa wanawake walioshindwa kupata watoto au wenye tatizo la kizazi.
Hata hivyo, baba Kanumba alimalizia kwa kusema kuwa, ingekuwa zamani ilikuwa ni kurithiwa tu lakini kwa sasa mila hizo zinapingwa vikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni