Ankal akiwa na Mkurugenzi Fredy Njeje katika jengo la Tone House ambamo kuna mambo kibao ikiwa ni pamoja na studio za Tone Radio-TZ lililopo Mwenge jijini Dar es salaam. Hapa ndipo nyumbani pa libeneke la Blog za Mikoa kama vile Mbeya Yetu, Lindi Yetu, Mwanza Yetu na kadhalika. Hawa vijana pia ni wanachama waanzilishi wa Tanzania Bloggers Network (TBN) ambayo inazidi kukua siku hadi siku... Haya si maneno yetu ni Maneno ya Ankali Mwenyewe.
Ankal Issa Michuzi Kutoka Michuzi Media Group ambao ni Wamiliki wa Michuzi Blog pamoja na Michuzi TV Jana alitembelea Makao makuu ya Tone Multimedia Group (Tone House) na kujionea Shughuli mbalimbali ambazo wanazifanya, na baadhi yake amezitaja hapo juu, Pia alipata nafasi ya Kuona Studio za Kurushia matangazo ya Online ya Tone Radio-Tz
Hii ilikuwa ni Ziara Muhimu kwa sababu tulijifunza mengi na Kubadilishana uzoefu. Asante kututembelea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni